Go to full page →

Njozi ni ya Hakika, Sura ya 58 Mar 66

Maana njozi hii ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Habakuki 2:3. Mar 66.1

Imani iliyomtia nguvu Habakuki, watakatifu na wenye haki siku zile za majaribio magumu ni imani ile ile inayotunza watu wa Mungu leo. Katika nyakati zilizo na kiza kabisa, katika mazingira yasiyo mazuri kabisa, Mkristo muumini aweza kudumisha muunganiko kati ya roho yake na chanzo cha nuru na uwezo. Siku kwa siku, kwa njia ya imani kwa Mungu, tumaini lake na ujasiri vyaweza kufanywa upya tena.... Katika huduma kwa ajili ya Mungu hakutakuwa na kukata tamaa, kusitasita, wala hofu. Bwana atatimiza matarajio ya juu zaidi ya wale wawekao tegemeo lao kwake. Atawapa hekima inayohitajika kulingana na mahitaji yao mbalimbali. Mar 66.2

Mtume Paulo anatoa ushuhuda juu ya uwepo wa mahitaji kwa wingi kwa ajili ya roho inayojaribiwa. Yeye alipewa uhakika wa kimbingu, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.” Kwa shukrani na ujasiri mtumishi wa Mungu aliyejaribiwa aliitikia: “Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha na shida, kwa ajili ya Kristo. Kwa maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” 2Kor. 12:9, 10. Mar 66.3

Tunapaswa kuiendeleza na kuijenga imani ambayo manabii na mitume wameishuhudia - imani ambayo anakamata ahadi za Mungu na kusubiri ukombozi katika wakati aliouamuru na njia aliyoipanga. Neno la hakika la unabii Iitatimilika mwishoni katika ujio wenye utukufu wa Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Wakati wa kusubiri waweza kuonekana kuwa mrefu, roho yaweza kuelemewa na matukio ya kukatisha tamaa, wengi ambao watu wamewaamini waweza kuanguka; lakini hebu tuungane na nabii aliyediriki kutia moyo Yuda wakati wa uasi mkubwa sana, kwa kusema, “. . .Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu: dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.” Mar 66.4

Hebu daima tukumbuke ujumbe huu unaochangamsha, “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. . . mwenye haki ataishi kwa imani yake.” Mar 66.5