Go to full page →

Sura ya Nane—KUKUA KATIKA KRISTO NA KUWA WATU WAKAMILIFU WAKE HUK 30

Kule kuongoka moyo ambako kunatufanya tupate kuwa watoto wa Mungu, kumenenwa katika Biblia kama ni kuzaliwa. Pengine tena kumelinganishwa na kuota kwa mbegu njema zilizopandwa na mlimaji. Vivyo hivyo wale ambao wameongoka moyo na kuanza kumfuata Kristo ni kama “watoto wachanga,” (1 Pet.2:2), tena lazima wakue hata wawe kama watu wazima katika Kristo Yesu. Kadiri zinavyotakiwa mbegu’ njema kwa mimea mizuri, basi pia imewapasa watu wawe na mbegu njema moyoni ili watoe matunda mema ya kiroho. Isaya asema juu yao, “Wapate kuitwa miti ya haki, miche ya BWANA, atukuzwe.”Isa.61:3. HUK 30.1

Akili zote na ustadi wote wa binadamu haviwezi kamwe kuhuisha kitu cho chote ulimwenguni. Hata wanyama wala mimea, yote hupata kuhuishwa na Mungu tu. Hivyo wanadamu hawapati kuzaliwa mara ya pili na kupata uzima mpya wa kiroho ila katika uzima utokao kwa Mungu. Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kushiriki uzima ule ambao hutolewa na Kristo. HUK 30.2

Na jinsi ilivyo katika kupata uzima, ndivyo ilivyo katika kuendelea kukua. Mimea haipati maua na matunda yake ila kwa uwezo wa Mungu tu. Yeye ndiye anayeziotesha na kukuza mbegu,“kwanza jani, tena suke, kisha ngano mpevu katika suke.” Marko 4:28. Mimea haikui kwa kuhangaika na kujitahidi yenyewe, ila kwa kuvipokea vile inavyopewa na Mungu kwa kuendesha uzima wako. Hivyo pia mtoto hawezi kuongeza urefu wake kwa kujitahidi mwenyewe. Na wewe pia, kwa kujishugulisha na kuhangaika kwako, huwezi kuendelea kukua katika mambo ya kiroho. Mmea wala mtoto hupata kukua wakipokea vile vinavyowoza kusaidia na kuendesha uzima wao, - hewa, jua na chakula. Na kwa kadiri vitu vile vikuwavyo kwa kuendesha uzima wa sasa, ndivyo akuwavyo Kristo kwa walo waaminifu wake. Yeye ndiye “nuru ya milelo” kwao, “ndiyo jua na ngao.” Atakuwa kama umande kwa Israel.” “Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa.” Yeye ndiye maji ya uzima, “mkate wa Mungu. . .ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.” Isa.60:19; Zab;84:11; Hosea 14:5; Zab.72:6; Yoh.4:14; 6:35,33. HUK 30.3

Yesu mwenyewe hufundisha mambo haya haya anaposema, “Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu.....Maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno.” Yoh.15:4,5. Tawi lazima lifungamane na mti wenyewe ili lipate kukua na kuzaa matunda; basi, pia imekulazimu kumtegema Kristo ili upate kuishi maisha safi. Pasipo yeye huna uzima kabisa. Peke yako huwezi kuyakinga majaribio, wala kukua kwa namna ya kiroho kuwa mtu mwenye usafi. Unapokaa ndani yake utasitawi. Kana unaishi kwake, huwezi kunyauka wala kutozaa matunda. Bali utakuwa kama mti uliopandwa mtoni penye naji. HUK 30.4

Wengi hudhani kwamba ni wajibu wao kufanya sehemu ya kazi ile wenyewe. Wamemtumainia Kristo kwa kusamehewa dhambi, lakini sasa waona kwamba ni heri wajitahidi wenyewe ili waishi maisha yaliyo sawa. Kujitahidi hivyo hakutafaulu kamwe, Yesu asema, “Pasipo mimi hamwezi kufanya neno.” Tena ni kwa njia ya kushiriki naye na kuongea naye, kwa kukaa ndani yake kila siku, saa zote, tunapata kukua kwa namna ya kiroho. Yeye si mwanzo tu wa imani yetu, ila mwisho wake pia; yaani, imetupasa kumtumainia Kristo tangu mwanzo mpaka mwisho. Imetupasa ili Kristo akae nasi si kwa siku zile tuanzapo kumjua na siku za mwisho wa maisha yotu, ilakini kwa mwenendo wetu wote katika maisha yotu yote. Daudi alisema, “Nimemweka BWANA sikuzoto mbele yangu: kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikitika.” Zab.16:8. HUK 30.5

Pengine unauliza,“Naweza je kukaa ndani yako Kristo ?” Kama vile ulivyompokea moyoni mara ya kwanza. “Kama nlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enondeni vivyo hivyo katika yoyo.” “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Wakol.2:6; Waeb.10:38. Ulijitoa kwa Mungu kuwa mtu wake kabisa, kumtii na kumtumikia, tena ulimtumaini Kristo kama Mwokozi wako. Wewe mwenyewe hukuweza kujiondolea dhambi zako na kugeuza moyo wako; lakini ulipokuwa umejitoa kuwa wa Mungu, ndipo ukasadiki kama Mungu ndiye aliyekutendea haya yote kwa ajili ya Kristo. Kwa njia ya kumwamini Kristo, ulikuwa wake; tena kwa kumwamini hivyo utazidi kukua nayo - kwa kujitoa na kupokea.Lazima ujitoe kwake kabisa, - moyo wako, nia yako, na utumishi wako; jitoe kwake na kuzishika amri zake na matakwa yake yote.Hivyo pia imekupasa kuvipokea vyote vinavyotoka kwa Kristo, ili akuwezesho kumtii sawasawa; ukubali Kristo mwenye mibaraka yote akae moyoni mwako, awe uwezo wako, na haki yako, na nsaidizi wako dum daina. HUK 31.1

Jitoe kwake Mungu kila asubuhi, kabla hujafanya kitu cho chote. Omba hivi: “Bwana wangu, unichukue, niwe wako kamili. Nia yangu na maazimio yangu yote nayaweka mbele yako. Unitumio leo, niwe mtumishi wako. Ukae nami ili kazi yangu yote itendeke kwa uwezo wako.” Hili ni jambo lipasalo kwa kila asubuhi, kujitoa kuwa wa Mungu kwa siku ile. Makusudi yako yote na niradi yako yote uweke nbele yake ili kuyafanya au kutoyafanya kwa jinsi atakavyckuonyesha. Hivyo ndivyo maisha yako yatakavyokuwa mkononi mwa Mungu kila siku, na maisha yako yatazidi kuwa kwa mfano wake Kristo. HUK 31.2

Kukaa ndani ya Kristo ni kukaa raha mustareho moyoni, na kutuliwa roho. Matumaini yako si juu yako mwenyewe, ila kwa Kristo. Udhaifu wako unefungamana na nguvu zake, ujinga wako na kutojua kwako hufungamana na akili zake, uhafifu wako na uwezo wake. Hivyo haifai kujiangalia nafsi na kujiwazia sana; yapasa kumwangalia Kristo tu, na kufikiri sana juu ya upondo wake na sifa yako jinsi ilivyo njoma na tinilifu. Jinsi Kristo alivyojinyima, na udhilifu wake jinsi alivyoaibiwa, jinsi olivyo safi na mtakatifu, upondo wake usio na kifani, - hayo ndiyo mambo yafaayo kufikiriwa moyoni. Kwa njia ya kumpenda, kumfuatisha kwa nejina ya matendo yako na tabia zake, kumtegomea na kumtumalnia kabisa, utapata kugeuka kuwa katika rnfano wako. HUK 31.3

Yesu asema, “Kaeni ndani yangu.” Maneno haya yatufikirisha juu ya kukaa mustarehe na imara, na kuwa na matumaini. Asema tena, “Njooni kwangu, nami nitwapumzisha.” Mattayo 11:28,29. Mtunga Zaburi alisema hivi: Umnyamalie BWANA, ukamngoje.;,Zab.37:7. Na Isaya pia butuambia, “Kwa kunyanaza na kutumaini zitakuwa nguvu zenu.” Isa,30:15. Kustarehe huku hakupatikani kwa kukaa bure katika hali ya kutofanya kazi; kwa kuwa katika maneno yale ya Mwokozi wetu, ahadi ya kupata raha imeungamana na wito wa kufanya kazi. “Jitieni nira yangu,...nanyi mtapata raha.” Mattayo 11:29 Yule anayemtegemea Kristo zaidi na kukaa raha kwake moyoni, ndiye atakayekuwa mtu wa moyo na juhudi kwa kumtunikia Mungu. HUK 32.1

Kama mtu anajifikiria nafsi na kujipendeza nwenyewe tu, roho yake hugeukia na kutoka kwa Kristo ambaye ni uwezo na uzima wake. Kwa hivyo Shetani huwa anafanya bidii kuvuta watu na kuwapotosha, ili kuwazuia wasimshiriki Kristo. Anasa za dunia, fadhaa na mashaka, ana huzuni, nakosa ya wengine, nakosa na upungufu wako mwenyewe - Shetani hutumia hayo yote kwa kupotosha fikara za watu. Tujiangalie tusidanganywe na hila zake. Wengi watako kufanya yapasayo na kuishi maisha safi machoni pa Mungu, mara nyingi huvutwa kwa Shetani katika kufikiri sana juu ya nakosa yao na udhaifu wao mpaka wame jitenga mbali na Kristo. Tusifikiri nafsi zotu sana, na kuhangaika na mashaka moyoni kama tutaokoka au sivyo. Mambo kama hayo hugeuza moyo kutoka kwa Kristo aliye asili ya nguvu zetu. Weka roho yako nkononi nwa Mungu kana amana, na kumtumainia. Mazungumzo yako na fikara zako ziwe juu ya Yesu. Uswe na shaka wala hofu moyoni, Sena kana alivyosema mtume Paulo, “Ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika nwili, ninao katika inani ya Mwana wa Mungu aliyeniponda akajitoa nafsi yako kwa ajili yangu.” Wagal.2:20 Ukae na kustarehe kwa Mungu, ukasadiki kwamba aweza kukilinda kilo ulichokiweka anana kwake. Kana unajiweka nkononi mwake, atakuwezesha kushinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyekupenda. HUK 32.2

Kristo alipoutwaa mwili wa kibinadamu, alijifungia mioyo ya wanadamu kwake kwa upondo wake, na kufungamana huku hakukuweza kuharibika ila kwa hiari ya mwanadamu nwonyewe. Shetani hufanya bidii sikuzote kuvuta roho zetu na kutushawishi ili tujitenge mbali nayo Kristo. Kwa hivyo imetupasa kujilinda, na kuomba kwa bidii ili tusishawishwe na jambo lo lote na kuchagua kutawaliwa na Shetani. Tumkazie Kristo macho yetu, yeye awozaye kutulinda. Tukintazama Yesu, tutakuwa salama; wala hekuna awezaye kutupokonya katika mkono wake. ‘Tukimwangalia Yesu na utukufu wake daima, “tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliyo Roho.” 2 Wakor.3:18. HUK 32.3

Hivyo ndivyo wanafunzi wake wa zamani walivyopata kufanana naye. Walikuwa naye wakafundishwa kwake. Wakamwangalia, kama watumishi wanavyomwangalia bwana wao, wapate kujua yaliyo wajibu Wao. Walikuwa wanadamu wenye “tabia moja na sisi.” Yakobo 5:17. Wakawa wakishindana na maovu sawa na sisi. Iliwapasa kusaidiwa kama sisi, wapate kuishi maisha yaliyo safi na matakatifu. HUK 32.4

Na hata Yohana, mwanafunzi mpendwa wa Yesu, aliyefanana naye zaidi ya wengine, hakuwa na sifa njema kwa desturi. Alikuwa mtu wa kujitokeza mbele na kutaka makuu. Naye alipozidi kufahamu namna ya sifa ya Yesu jinsi ilivyo bora, alizidi kuona upungufu wake mwenyewe na kushushwa moyo. Siku kwa siku moyo wake ukazidi kuvutwa kwake Yosu Kristo, na kujisahau nafsi yake mwenyewe. Moyo wake ulitengenezwa kuwa mpya kwa Roho Mtakatifu, na hata tabia zake hasa ziligeuka kufanana naye Kristo. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa kila ashirikianaye na Yesu. Kristo akaapo ndani ya moyo, na kuutawala, ndipo yule mwanadamu hugouzwa tabia zake hasa, na fikara zake na matamani yake yakuwa juu ya Mungu na mambo ya mbinguni. HUK 33.1

Siku ya kupaa mbinguni, Yosu aliwaambia wanafunzi wake, “Tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote , hata mwisho wa dunia.” Mattayo 28:20. Akapaa mbinguni na umbo wa binadamu. Walijua ya kwamba alikwenda kuwaandalia makao, na kurudi tena baadaye, kuwapeleka kwako alipo. HUK 33.2

Walipokutana walikumbuka ahadi yake. jinsi alivyosema, “Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni. Mpaka leo hamkuomba nono kwa jina langu; ombuni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu.” Yoh.16:23,24. Pia walitumaini ya kwamba “Kristo ndiye aliyekufa, naan, na zaidi ya haya, amefufuka, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anayetuonbea.” Warumi 8:34. Na siku ya Pontekote wakapata kujazwa Roho Mtakatifu, yule Mfariji ambaye Kristo alisema juu yake, “Naye atakaa ndani yenu.” Alisema pia, “Yawafaa ninyi niondoke; kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikionda zangu, nitampeleka kwenu.” Yoh.l4:17; 16:7. Tangu siku hiyo, kwa njia ya Roho Mtakatifu, Kristo amokuwa anaweza kukaa mioyoni nwa watu wako sikuzote. Sasa waweza kumshiriki Kristo zaidi kuliko walivyomshiriki siku zile alipokuwa nao katika umbo wa binadamu. Upondo na uwezo wa Kristo vikaonekana kwao, hata wengine walipotambua hivyo, “watastaa jabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.” Matendo 4:13. HUK 33.3

Kwa kadiri Kristo alivyowasaidia wanafunzi wake wa zamani, ndivyo atakavyo kuwasaidia watu wake wa sasa; kwa kuwa katika kuomba kwako alisema, “Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.” Yoh. 17:20. HUK 33.4

Yesu alituombea sisi, ili tuwo katika umoja ndani yake, kama yeye na Baba yake walivyo katika umoja. Huo ni umoja wa namna gani! Mwokozi alisema juu yake mwenyewe, “Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, ila lile amwonalo Baba analitonda;” akasema tena, “Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.” Yoh.5:19; 14:10. Ikiwa Kristo anakaa mioyoni mwetu, atatenda kazi yake ndani yetu, ili kutaka kwetu na kutonda kwetu kupatana na kusudi lake jema. Wafil.2:13. Tutafanya kama alivyofanya yeye; tutakuwa na nia ndani yetu iliyokuwamo ndani yake; hivyo kwa kumpenda na kukaa ndani yake, tutakua “mpaka tumfikie yeye katika yote, aliye kichwa, ndiyo Kristo.” Waof.4:15. HUK 33.5

Furaha gani na ushiriki
Nikintegomea Yesu tu!
Baraka gani, tona amani,
Nikimtegemoa Yosu tu!

Togemea,
Salama bila hatari;
Tegemea,
Togomoa Bwana Yosu tu.

Nitaiwoza njia nyombamba,
Nikimtogomea Yosu tu;
Njia tazidi kuwa rahisi,
Nikimtegemea Yesu tu.

Sina sababu ya kuogopa,
Nikimtegemea Yesu tu;
Atakuwa karibu daima,
Nikimtegemea Yesu tu. HUK 34.1