Kwa njia nyingi Mungu anajaribu kutujulisha tabia zake, tupate kumjua na kushirikiana naye. Viumbe vya ulimwengu vyatuonyesha wema na upendo wake milele. Moyo unaofunuliwa utaona upendo na utukufu wa Mungu jinsi unavyconekana katika matendo yake na katika kazi za mikono yake. Tukiona na kufikiri juu ya miti na maua, mazao ya mashamba, mawingu, mvua, mito, nyota na uzuri wote wa mbingu, hatuna budi kuvutwa moyoni kumjua yeye aliyeviumba vyote. HUK 38.1
Mwokozi wetu alitoa mafundisho mengi juu ya viumbe vya ulimwengu. Akasema juu ya miti, maua, ndege, vilima, maziwa ya maji, na vitu vya mbinguni, pamoja na mambo yanayowatukia watu katika maisha yao sikuzote; na watu walipoviona vitu vile na mambo hayo mara kwa mara iliwalazimu kukumbuka mafundisho yake. HUK 38.2
Tukifunua roho zetu na kusikiliza sauti ya Mungu katika viumbe vyaake, tutapata kufundishwa namna ya kumtii na kutawakali kwa Mungu. Viumbe vyote, tangu nyota zinazofuata njia zao mbinguni, hata na vidudu vidogo, vyote hufuata mapenzi ya Mungu. Tena Mungu huangalia kila kitu alichokiumba. Huzitegemeza nyota katika mahali pakubwa mbinguni, na hata ndege wadogo wa anga huangaliwa naye. Wanadamu wakiondoka asubuhi kwenda kazini, na wakati waombapo, wakati wanapokwenda kulala usiku; tajiri katika jumba lake, hata na maskini katika kibanda chake, Baba yetu aliye mbinguni huwaangalia wote kwa huruma na upendo. Mtu akitoka machozi ama akiwa na furaha, Mungu huona yote. HUK 38.3
Kama tungesadiki hivyo kabisa, mahangaiko yote yasiyofaa yangeondolewa mioyoni mwetu: kwa sababu mambo yote, makubwa hata madogo, yangekuwa tunayaacha mkononi mwa Mungu; nasi tungeona raha mioyoni mwetu. HUK 38.4
Na kama unapendezewa macho kwa kuona uzuri wa dunia hii, fikiri juu ya ulimwengu mpya ujao, ambao huko uharibifu wa dhambi na mauti hautaonekana kamwe. Tena ukumbuke kwamba fahari na utukufu vyake havina kifani. Imeandikwa, “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1 Wakor.2:9. Hakuna awezaye kufurahiwa na kutambua uzuri wa viumbe vya ulimwengu kama yeye aonaye kuwa vyote hutoa habari jinsi Mungu anavyowapenda wanadamu. HUK 38.5
Mungu huseme nasi katika matendo yake, pia katika maongozi yake, tena katika mvuto wa Roho yake mioyoni mwetu. Katika mambo yanayotukia kwetu, na katika hali yetu, twaweza kupata mafundisho yake, ikiwa mioyo yetu imekuwa wazi kuyatambua mafundisho yake Mungu. Mtunga Zaburi alisema, “Nchi imejaa wema wa Bwana.” “Mwenye hokima atayaangalia haya, nao watazijua rehema za Bwana.” Zaburi 33:5; 107:43. HUK 38.6
Mungu husema nasi tena katika Neno lake. Hapo imefunuliwa dhahiri sana namna ya sifa yako na tabia zake, jinsi anavyowatendea wanadamu, na kazi yake kubwa katika kuwakomboa wanadamu. Hapo zimesimuliwa habari za wazee wakuu na manabii na wengine wa zamani waliokuwa watu wa Mungu. Hao nao wakawa watu wenye “tabia moja na sisi.” Yakobo 5:17. Twasoma juu yao jinsi walivycshindana na mambo ya kulegeza moyo kana sisi tunavyolazimishwa kushindana; walijaribiwa na kuvutwa na mabaya kana sisi tunavyopata kuvutwa; hata hivyo walijitia noyo tena, wakashinda kwa uwezo na neena ya Mungu; na sisi pia tukijua hivyo imetupasa kujitia noyo na kuendelea kujitahidi katika kuyanyosha maisha yetu ili yawe na haki machoni pa Mungu. Kama tunaona namna ya kazi wale watu wa zamani waliyofanya kwa neena na msaada wa Mungu, na jinsi walivyobarikiwa na kupata furaha katika kufanya kazi ile, sisi pia twatamani kufanana nao kwa namna ya sifa yao, na kuendelea pamoja na Mungu kama wao. HUK 39.1
Maandiko Matakatifu hutoa habari za Kristo, jinsi alivyosema,“na hayo ndiyo yanayonishuhudia,” Yoh.5:39. Biblia nzima hutoa habari za Kristo. Tangu habari za mwanzo juu ya kuumba kwa ulimwengu - kwa kuwa “pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika”, Yoh.1:3 - mpaka ahadi ya mwisho,“Angalieni, nakuja upesi”, Uf.22:12, twasoma juu ya matendo yake tena twasikiliza sauti yake. Kama unataka kumjua yule aliye Mwokozi, heri wufanye bidii katika kuyachunguza maneno ya Biblia, yaani Maandiko Matakatifu. HUK 39.2
Ujaze moyo mzima maneno ya Mungu. Hayo ndiyo maji ya. uzima, na mkate wa uzima utokao juu. Yesu alisema,“Msipoila nyama yako Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.” Akazidi kueleza maana yake hivi:“Maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.” Yoh.5:53,63. Kadiri miili yetu inavyokuwa mizima na kupata afya njema kwa ajili ya vile tulavyo na tunywavyo, basi vivyo hali yetu ya kiroho itazidi kuwa njema na kuongezeka nguvu kwa vile tunavyofikiri na kuwaza mambo ya kiroho. HUK 39.3
Jambo la ukombozi wetu katika Kristo ndilo jambo ambalo malaika wanatamani kulichungulia; tena litakuwa jambo kuu katika kuelimisha wateule wa Mungu katika ufalme wake hata milele. Je, si jambo lifaalo kufikiriwa hata na sisi katika zamani hizi ? Imetupasa kufikiri sana juu ya rehema na upendo wa Yesu, na jinsi alivyojitoa maisha yake kwa ajili yotu. Imetupasaa kuchunguza sifa na tabia za Mwokozi wetu. Ni wajibu wetu kufikiria kazi yake katika kuwaokoa watu wake katika dhambi zao. Na tunapowaza mambo matakatifu, imani yetu na upendo wetu vitaongezeka kwake, tena kwa hiyo maombi yetu yatazidi kukubaliwa na Mungu. Tutazidi kumtegemoa na kumtunainla Kristo na uwezo wake “kuwaokoa kabisa wao wa jao kwa Mungu kwa yeye.” Waeb.7:25. HUK 39.4
Na tunapofikiri juu ya Mwokozi jinsi alivyo mkamilifu mwenye sifa bora, tutatamani kugeuka moyo kuwa wapya na kufanana naye hasa katika usafi wake, Tena tukizidi kumfikiri Kristo, tutazidi kumshuhudia kwa wengine. HUK 40.1
Biblia haikuandikwa kwa wenye elimu nyingi tu; bali ilikusudiwa kuwa ya watu wote, hata na akina sisi. Mafundisho makubwa na wokofu yamekuwa dhahiri kabisa, na mtu ye yote aweza kuyafahamu; hakuna awezaye kukosa njia ya haki ila yeye afuataye nia yake mwenyewe badala ya kufuata mapenzi ya Mungu. HUK 40.2
Tusikubali neno lo lote la binadamu juu ya mafundisho ya Eiblia, bali tujifunze wenyewe maneno ya Mungu na kuyachunguza hata tumefahamu maana yako. Tukifanya bidii katika kujifunza mambo ye Biblia, tukilinganisha sehemu fulani ya Biblia na sehemu nyingine, na mambo ya kiroho na mambo ya kiroho, tutaona kuwa akili zetu zinaongezeka. HUK 40.3
Hakuna njia nyingine ya kuzidisha akili zaidi ila ya ku-jifunza na kuyachunguza maneno ya Biblia. Mafundisho yake yaweza kuadilisha fikara na kuzidisha akili kwa namna isiyowezekana kwa kusoma kitabu kingine cho chote. HUK 40.4
Kama wanadamu wange jifunza na kulichunguza Neno la Mungu kama inavyostahili, wangekuwa na maarifa mengi na sifa bora, na kuimarishwa moyoni. HUK 40.5
Lakini hakuna faida katika kusoma Biblia ovyo ovyo kwa haraka. Kwa namna hiyo tungeweza kuisoma Biblia nzima bila kutambua uzuri wake wala kufaliamu maana yake, hasa maana ya siri ya ndani. Yafaa kuisoma sehemu moja na kuichunguza sana mpaka maana yake imekuwa dhahiri, na kuona jinsi inavyohusiana na mpango wa Mungu kwa kuwaokoa wanadamu; kufanya hivyo kwa kila sehemu ya Biblia kutakuwa faida sana kuliko kusoma tu sura nyingi bila kusudi la kujifunza hakika yake. Biblia yako iwe karibu nawe kila mara. Kila upatapo nafasi, isome; jifunza mafungu yake kwa moyo. Hata wakati utembeapo, waweza kulisoma fungu fulani na kulifikiri maana yake, na kulitia moyoni. HUK 40.6
Hatuwezi kupata kuelimishwa bila kujitahidi na kukaza moyo kwa kujizoeza kusoma pamoja na kuomba. Kuna sehemu nyingi za Biblia ambazo maana yake imekuwa dhahiri kabisa; lakini kuna sehemu nyingine tena ambazo maana yake si rahisi kufahamiwa mara moja. Yapasa kulinganisha sehemu moja na sehemu nyingine, na kuzifikiri na kuzichungua sana pamoja na kuomba. Tusifungue kabisa Biblia na kuyasoma maneno yake bila kuomba. Kabla ya kuifungua Biblia heri tusali ili tupate mwangaza wa Roho Mtakatifu, ndipo tutaupata. Nathanael alipomwondea Yesu, Mwokozi alisema,“Tazama, huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.” Nathanael akamwambia, “Umepataje kunijua ?” Yesu akamjibu, “Kabla Filipo hajakuit, ulipokUwa chini ya mtini, nalikuona.” Yoh.l:47,48. Tena Yesu ataonana nasi katika mahali pa siri pa sale, ikiwa tutamwomba ili tupste kueliraishwa na kujua yaliyo ya kweli. Malaika watokao mbinguni watawasaidia wale watakao kuongozwa na Mungu. HUK 40.7
Roho Mtakatifu humtukuza na kumsifu Mwokozi. Kazi yake ni kutuonyesha Kristo, na hali yako jinsi ilivyo yenyu haki na usafi, na kutudhihirisha habari za wokofu tupatao kwake. Yesu alisema, “Atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni habari.” Yohana 16:14. Roho ya kweli ndiye mwalimu wa pekoe awezaye kutujulisha barabara yaliyo kweli ya Mungu. Ni dhahiri kama Mungu huona wanadamu kuwa wa thamani kubwa, kwa kuwa alimkubali Mwanawe afe kwa ajili yetu, tena ameweka Roho yake Mtakatifu kuwa mwalimu na kiongozi wa wanadamu daima. HUK 41.1
Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu;
Nijue pondo lake, na
Wokofu wako kamili.
Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.
Nataka nifahamu, na
Nizidi kupambanua
Mapenzi yake, nifanyo
Yale yonayompendeza.
Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyashe
Wengine wokofu wake. HUK 41.2