Watu wa Mungu wameitwa wajumbo wa Kristo, kwa kutangaza wema wa Bwana na rehema zake. Kwa vile Yesu alivyotudhihirishia sifa za Baba, hivyo na sisi imetupasa kuwadhihirishia wengine wasiomjua Kristo jinsi alivyo mwenye upendo, mwenye huruma. Yosu alisema, “Kama ulivyonituma mimi ulimwonguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwonguni.” “Mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, ...ili ulimwengu ujuo ya kuwa ndiwe uliycnituma. Yoh.17:18,2,3. Mtume Paulo huwaambia wanafunzi wa Yesu, “Mnadhihirishwa kuwa ni barua ya Kristo,” inavyojulikana “na kusomwa na watu wote.” 2 Wakor.3:3,2. Kila mmoja wa watoto wake ni kama barua Yesu anayoipeleka ulimwenguni. Kama wewe mfuasi wa Kristo, ndiwe barua yake anayoipeleka kwa jamaa zako, nji wako, na mtaa unaokaa. Yesu akaapo ndani yako, anataka kusema kwa mioyo yao wasiomjua. Pengine hawasomi Biblia na kusikia sauti yake humo; hawatambui upendo wa Mungu kwa kuumba kwake. Lakini kama wewe ni mjumbo wake wa kweli, pengine kwa sababu ya mwonendo wako mwema na matendo yako noma, wataongozwa wapate kujua kidogo wema wake na kuvutwa kwake Yesu, hata kwapenda na kumtumikia. HUK 51.1
Wakristo wamewekwa kuwaangaza wengine njia iendayo mbinguni; kuwaonyesha nuru itokayo kwa Kristo. Mienondo yao na sifa yao yapasa kuwa safi, kuwajulisha wengine hakika ya Kristo na namna ya kumhudumia. HUK 51.2
Nasi tukiwa wa jumbe wa Kristo kweli, tutakuwa watu wa furaha. Wakristo ambao huzoea kuwa na moyo mzito, wagunao na kunung unika, huonyesha wengine mfano usio wa kweli juu ya Mungu na maisha ya kikristo. Wale ambao mienendo yao na desturi zao zinafanya wengine kudhani kwamba Mungu hapendezwi kama watu wake wakifurahi, hao nao wananshuhudia uwongo Baba yotu aliye mbinguni. HUK 51.3
Shetani husimanga sana kama anaweza kuwatilia watu wa Mungu fikara za kutoamini na kufa moyo. Hufurahi sana tukiona mashaka moyoni juu ya Mungu jinsi anavyotupenda na kuweza kutuokoa. Ni kazi ya Shetani kutoa mfano wa Mungu kuwa asiye na huruma na rehema. Hujaribu kuutia moyo wa binadamu fikara za uwongo juu ya Mungu; nasi mara nyingi twasikiliza habari zile za uwongo, na kutomheshima Mungu kwa ajili ya kutomwamini na kunnung unikia. Shetani hujaribu kwatia watu fikara kuwa njia ya Kikristo ni ya taabu na shida. Tena Mkrist kama anaonyesha mashaka haya katika maisha yake, ni kama kusoma yu pamoja na Shetani. HUK 51.4
Wengi hufikiri sana makosa yao, upungufu wao na dhiki zao, hao nao mioyo yao hujaa huzuni na uchungu. Je, katika maisha yako hujapata mambo yafaayo kuyafurahia ? Hata nyakati nyingine ulipoona furaha moyoni mwako kwa ajili ya mvuto na uongozi wa Roho ya Mungu ? Hata hujaona uzuri wa ahadi za Mungu? HUK 51.5
Kudunu kufikiri mambo hayo yanayoutia moyo uchungu na kukata tamaa, ni kama kukusanya miiba na viwavi vinavyotuchoma na kutuuma, bila kuona maua na matunda jinsi yakuwavyo vizuri na kufurahishr moyo. Yule ambaye amekata tanaa, moyo wake umekufa ganzi, haoni nuru ya Mungu moyoni mwake, pia huwatia wengine giza njiani mwao. HUK 52.1
Tumshukuru Mungu kwa vile ambavyo ametuhakikishia upendo wake kwa njia nyingi zitupasazo kuzifikiri mara kwa mara; Mwana wa Mungu jinsi alivyoacha utukufu wake, na kuwa katika mfano wa kibinadamu apate kutuokoa katika mamlaka ya Shetani; jinsi alivyomshinda Shetani, na kuinua binadamu toka katika hali ya uhalifu ambayo aliangukia kwa ajili ya dhambi, nr. kutupatanisha tena na Mungu; naye binadamu akivumilia na kustahimili hata mwisho kwa kumwamini Mwokozi, jinsi atakavyovikwa nguo nyeupe, yaani haki itokayo kwa Mungu, kwa imani - hayo ni mambo ambayo Mungu ataka tuyafikirie. HUK 52.2
Ikionekana kwetu kama kwamba tuko katika hali ya kutosadiki upendo wa Mungu na ahadi zake, tunamdharau Mungu na kumhuzunisha Roho yake Mtakatifu. Mama fulani angeonaje kama watoto wake wangemnung unikia mara kwa mara kama asiyetaka kuwatendea vizuri, naye hudumu kuwafikiri na kuwatendea mema ? Na sisi je, Baba yetu aliye mbinguni ataonaje kama tunamdharau upendo wake jinsi alivyomtoa Mwana wake wa pekee ili tupate uzima ? Mtume Paulo alisema, “Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yotu sisi, atakosaaje kutukarimia na vitu vyote pamoja naye ?” Warumi 8:32. Hata hivyo kuna wengi ambao kwa matendo yao, si kwa maneno hasa, huwa wanasema, “Maneno ya Mungu haya hayanihusu mimi. Pengine awapenda wengine, lakini si mimi.” HUK 52.3
Katika kufanya hivyo unajihatarisha moyo wako mwenyewe; kwa kuwa kila mara unaposema maneno ya kushuku na kutoamini, unazidi kujithibitisha katika kutoamini; tena si wewe mwenyewe tu ambaye unajihatarisha kwa tendo hili; hata na wale ambao wanasikia maneno yako watavutwa kuwa na shaka pia, tena pengine haitawezekana kubatilisha matokeo ya maneno yako jinsi yatakavyokuwa mwishowe. Wewe mwenyewe labda utaweza kuokoka katika mteggo wa madanganyo ya Shetani, lakini walo waliovutwa kwako, pengine hawataweza kuondolewa mawazo yale uliyowatia mioyoni mwao. Hivyo inatupase sana kusema mambo yale tu yatakayozidisha nguvu na uzima wa kiroho! HUK 52.4
Watu wote hupata majaribu: mambo ya kutia me jonzi na huzuni, ambayo ni vigumu kuyastahimili; na mivuto ya Shetani, ambayo ni vigumu kuipinga. Tusiwasimulie wanadamu wenzetu taabu zetu na mambo ya kuwatia mashaka mioyoni mwao; ila tumwonyeshe Mungu shida yetu yote katika sala zetu. Kwa namna ya maisha na maneno yetu, wengine waweza kutiwa moyo na kuzidiwa nguvu, ama waweza kuingiliwa na mashaka na kuzuiwa wasimtako Kristo na ukweli wake. HUK 52.5
Ni kweli Mwokozi wetu alikuwa mtu wa huzuni, ajuaye taabu, kwa kuwa alichukua huzuni zote za wanadamu. Lakini i japokuwa hivyo, moyo wake ulikuwa mtulivu, nao ulikuwa kama chemohemi ya uzima; po pote alipokwenda, aliwatia watu raha, amani, furaha na shangwe mioyoni mwao. Alikuwa mtu wa moyo wa juhudi, asiye mtu wa chuki, wala mwenye uso mzito kamwe. Maisha yao wanaomfuata Mwokozi yatakuwa na kusudi jema; watafahamu jinsi walivyo na mzigo wa kuwa mfano wake mbele ya wengine. Hawatatoa ubishi na upuzi au kufanyiza mzaha, kwa kuwa dini ya Yasu ni adibu na ya utaratibu: ni dini ya amani. Dini hii haizimi furaha wala kuzuia ukunjufu au micheko ya upendo. Kristo hakuja kuhudumiwa bali kuhudumu; upendo wake ukiwa moyoni tutafuata mfano wake. HUK 52.6
Tukifikiri sana juu ya makosa ya wengine, ukali wao na matendo yao yasiyo na haki, haitawezekana kwetu kuwapenda jinsi Kristo alivyotupenda sisi. Ilakini tukifikiri zaidi juu ya pendo la ajabu na huruma ambavyo Kristo anatuonesha sisi, haitakuwa vigumu kwetu kuonyesha roho ileile kwa wengine. Tungependana na kuheshimiana ingawa tunajuana kuwa na makosa. Tungejifunza kujidhili na kuwa na unyenyekevu na kuyavumilia makosa ya wengine kwa upole mwingi. Hivyo upendo mkuu wa nafsi zetu utatoka na tutajaa ukarimu wa moyo. HUK 53.1
Mtunga Zaburi asema, “Umwamini Bwana, ukatende mema; ukae kwa nchi, ukaishike amini.” Zab.37:3. “Umwamini Bwana.” Kila siku inaleta taabu na mahangaiko yake; nasi tu wepesi kuzungumza na wenzetu juu ya shida zetu na majaribu yetu, kana kwamba hatuna Mwokozi atupendaye, aliye mwepesi kusikia haja zetu zote, naye karibu sana kutusaidia katika shida. HUK 53.2
Wengine huzoea kuwa na hofu na kutazamia shida isiyokuwapo bado. Sikuzote sisi huzungukwa na vitu vinavyoonyesha upendo wake; kila siku hufurahiwa na wingi wa majaliwa ya Mungu; lakini wengine wetu husahau mibaraka ya sasa hivi, na huzoea kufikiri mabaya wanayodhani labda yatakuja. HUK 53.3
Je, imetupasa kutokuwa na shukrani na amini hivi ? Yesu ndiye rafiki yetu. Wa mbinguni wote hutufikiri sisi. Tusife moyo; tumtwike Bwana taabu zetu zote, nasi tuwe na amani na uchangamfu. Tumwombe Mungu hekima na akili katika kufanya shughuli yetu, tusipate hasara na misiba. Yesu ameahidi msaada wake, lakini inatupasa pia tufanye juhudi sisi wenyewe. Si mapenzi ya Mungu sisi tutaabike. Bwana wetu hatudanganyi. Hasemi, “Msiogope; hamtapata kuhatirishwa kamwe.” Si kusudi lake kuwatoa watu wake katika dunia palipo dhambi na maovu, lakini huwaonyesha mahali pa kukimbilia kwa kupata msaada. Aliwaombea wafuasi wake hivi: “Siombi uwatoe katika ulimwengu, bali uwalinde na yule mwovu.” Alisema pia, “Ulimwenguni mtapata shida: lakini jipeni moyo: mimi nimeushinda ulimwengu.” Yoh.17:15; 16:33. HUK 53.4
Katika mafundisho yake mlimani, Kristo aliwafundisha wafuasi wake kwamba ni lazima kumtumaini Mungu. Mafundisho haya yalikusudiwa kusaidia watu wa Mungu sikuzote hata zamani hizi ili wajipe moyo. Mwokozi aliwaonyesha ndege za anga, jinsi waimbavyo bila kufadhaika moyo; “hawapandi, wala hawavuni.” Lakini Baba aliye mbinguni awalisha. Ndipo Mwokozi anauliza, “Ninyi je! si bora kupita hao ?” Mattayo 6:26. Baba mkuu hufunua mkono wake, huviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao. Ndege hawana budi kudonoa punje za nafaka na vitu vinginevyo vinavyokuwa chakula chao. Imekuwa juu yao kuokota vitu vya kutengeneza vioto vyao. Wamelazimishwa kuwalisha watoto wao. Hao nao huondoka kufanya kazi yao na wimbo kwa kuwa “Baba yonu wa mbinguni awalisha ha.” na “ninyi je ! si bora kupita hao ?” Naye alituumba sisi katika mfano wako mwenyewe, nayo angekosa kuturuzuku mahitaji yetu kama tunamtumainia ? HUK 53.5
Kristo alielekeza nia za wafuasi wako kwa maua ya mashamba, jinsi yameavyo. Alisema kwamba “hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja la hayo.” Naye Yesu auliza, Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba ?” Mattayo 6:28,30. Fundisho hili la Kristo linakaripia masumbufu na mahangaiko ya moyo usio na imani. HUK 54.1
Mungu ataka watu wake wote wawe na moyo wa furaha na utulivu, na usikivu. Yesu alisema, “Amani nawaacheni; amani yangu nawatolea; si kama ulimwengu utoavyo, mimi nawatolea. Msifadhaike moyo weny, wala msiwe na woga.” “Haya nimewaambieni, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yonu itimizwe.” Yoh.14:27; 15:11. HUK 54.2
Furaha iliyotakiwa na mtu fulani kwa ajili ya kujipendeza mwenyewe, bila kufanya yaliyompasa, hiyo ndiyo furaha isiyofaa, isiyo na faida, furaha isiyodumu. Lakini katika kumhudumia Mungu, Mkristo aweza kupata furaha na kuridhishwa moyo. Ingawa tunakosa anasa za maisha haya, twaweza kuona furaha moyoni katika kutumainia maisha yajayo ya milele. HUK 54.3
Lakini hata hapa duniani Wakristo waweza kufurahi katika kumshiriki Kristo na kuongea naye; waweza kujua upendo wake, na kufarijiwa moyoni. Kila siku katika maisha haya ya sasa twaweza kuzidi kumkaribia Yesu na kuzidi kujua upendo wako jinsi ulivyo kwetu. Tusiutupe ujasiri wetu; bali tushikamane sana ” na ujasiri wetu,...kwa kutumaini mpaka mwisho.” Waeb. 10:35; 3:6. “Hata sasa Bwana ametusaidia,” pia atatusaidia mpaka mwisho. Heri tudumu kufikiri nanbo yaliyo ukumbusho kwotu, jinsi Bwana alivyotusaidia na kutuokoa nkononi mwako aliye mharabu. Tukizcea kukumbuka jinsi Mungu alivyotuhurumia - machozi ambayo ameyafuta katika macho yetu, maumivu yetu aliyoyatuliza, jinsi alivyotuondolea fadhaa na hofu mioyoni mwetu, jinsi alivyoturuzuku mahitaji yetu, na mibaraka yake ambayo tumeipata - tutajipa noyo kwa kujiweza kustahimili yote yatakayotupata katika siku zijazo. HUK 54.4
Katika mashindano ya yule mwovu yatakayokuwa kwa siku zijazo, twajua kwamb tutafadhaika moyoni; lakini kwa vile tunavyofikiri mambo yaliyopita na kusema, “Hata sasa Bwana ametusaidia,” twaweza kutazamia mambo yatakayokuja na kujua hivi: “Na kadiri ya siku zako kadhalika nguvu zako.” 1 Sam.7:12; Kumbu.33:25. Majaribu hayatakuwa makali kushinda nguvu tutakayopewa kuyastahimili. Kwa hiyo tushike kazi yetu jinsi ilivyo, na kutumaini kwamba tukipatwa na jambo lo lote, bila shaka tutapewa nguvu kwa kadiri ya jaribio lile ili tuweze kustahimili. HUK 55.1
Hatimaye milango ya mbinguni itafunguliwa kuwakaribisha wana wa Mungu, naye Mfalme wa utukufu atwaambia, “Njooni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu.” Mattayo 25:34. HUK 55.2
Ndipo waliokombolewa watakaribishwa hapo Yesu anapowaandalia. Hapo majirani wao hawatakuwa waovu wa dunia, wawongo, makafiri, wasio na usafi na wenye kutoamini; bali watashirikiana nao waliomshinda Shetani, wenye kufanana na Mungu na kuwa na sifa kamilifu. Kila tamaa ya dhambi, kila ukosefu na ila ambavyo tunavyo katika hali yetu ya sasa, vitakuwa vimefutwa na damu ya Kristo; hao nao watapata uzuri usio na kiasi na kuwa na utukufu wake Kristo. Watakuwa na sifa kamilifu kwake; watasimama mbele ya “kiti cha enzi, cheupe, kikubwa” wakiwa bila ila na mawaa. HUK 55.3
Kwa sababu ya utukufu wa urithi uliowekwa kwake, “mtu atatoa nini badala ya roho yake ?” Mattayo 16:26. Hata amekuwa maskini, mwana wa Mungu huwa na utajiri na heshima ambavyo haviwezi kupatikana kwa dunia. Moyo uliokombolewa na kusafishwa dhambi, na kujitoa kumtumikia Mungu, umekuwa wa thamani kubwa isiyokadiriwa; iko furaha mbele ya Mungu na malaika zake kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, furaha inayoonyeshwa kwa nyimbo za shangwe. HUK 55.4
Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi.
Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;
Na kwa utukufu wake nitamwona milele.
Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa;
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.
Mbelo yake yafukuzwa machezi na huzuni;
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.
Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;
Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi. HUK 55.5