Go to full page →

Ishara ya Mwongofu wa kweli TVV 153

Ili kusudi kutunza Sabato kamili, watu hawana budi kuwa watakatifu wao wenyewe. Kwa imani lazima wawe wenye kushiriki haki ya Kristo. Sheria ilipotolewa kwa Waisraeli kwamba “Ikumbube siku ya Sabato uitakase.” Kutoka 20:6. Bwana alisema pia kuwa, “nanyi mtakuwa watakatifu kwangu.” Kutoka 22:31. TVV 153.2

Jinsi Wayahudi walivyofarakana na Mungu, wala hawakupata haki ya Kristo kwa imani, Sabato ilipoteza umuhimu wake kwao. Shetani aliwaongoza kupotosha Sabato, kwa kuwa ni ishara ya uwezo wa Mungu. Viongozi wa Wayahudi waliiwekea Sabato mizigo mingi wakaifanya kuwa mzingo mzito kwa watu. Katika siku zile za Kristo ilionyesha tabia ya ufedhuli na ubinafsi kwa watunzaji wake badala ya tabia ya upendo wa baba wa mbinguni. Marabi walimwonyesha Mungu kama aliyewapa sheria isiyowezekana kushikwa, au kutiiwa. Waliwaongoza watu kumdhania Mungu kuwa asiyekuwa na huruma, na kuona kuwa Sabato ni ya ukatili. Ilikuwa kazi ya Yesu kusahihisha makosa haya. Kwa hiyo Yesu hakukubaliana na maongozi ya Marabi, ila aliendelea kuishika Sabato ya Mungu kwa kadiri ilivyo hasa. TVV 153.3