Go to full page →

Jinsi Nira yake inavyorahisisha kazi TVV 181

Nira huwekwa shingoni mwa dume la ng’ombe ili kurahisisha kazi ya kukokota mzigo. Ndivyo ilivyo na nira ya Kristo. Wakati mapenzi yetu yanapomezwa katika mapenzi ya Mungu, tutaona kuwa mzigo wa maisha huwa rahisi kubebeka. Mtu anayetembea katika njia ya Mungu na katika sheria zake, hutembea na Kristo, na katika upendo wake, roho kupata pumziko. Wakati Musa alipoomba kwamba, nionyeshe njia yako, ili nikujue wewe, Baba alimjibu, “Kuwako kwangu kutaenda pamoja nawe, na mimi nitakupa pumziko.” Kutoka 33:14. TVV 181.3

Watu wanaomchukua Kristo katika neno iake, na kujitoa kufuata anavyoagiza, watapata amani na burudiko. Hakuna kitu duniani kitakacho wahuzunisha, wakati Yesu atakapowafurahisha kwa kuwako kwake, “utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea;’ katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.” Isaya 26:3. TVV 181.4

Maisha yetu yaweza kuonekana kana wamba yana matatizo, lakini kadiri tunavyojitoa kwa Bwana mwenye hekima zote, atayarekebisha maisha yetu katika hali ifaayo, ambayo ni ya utukufu wake. Hali hiyo iliyo ya tabia yake ya utukufu, ndiyo itakayopokewa katika Paradiso ya Mungu. TVV 181.5

Kwa njia ya Yesu tutakapoingia katika pumziko, mbingu huanzia hapa. Tunaitikia mwito wake, kwamba: “Njoni, mjifunze kwangu,” na kwa njia hiyo tunaanza maisha ya umilele. Mbingu haikomi kuonekana kwa njia ya Kristo. Tunapomjua Mungu zaidi na zaidi, ndivyo tutazidi kuwa na furaha kuu. Kadiri tunavyotembea na Yesu katika maisha haya, tunaweza kujazwa na upendo wake, na kuridhika kwa kuwako kwake pamoja nasi. Mambo yote ^awezayo kupokelewa na binadamu hapa, tutayapokea. TVV 181.6