Go to full page →

Uchungu ambao Mama wa Kristo hana budi kuufahamu TVV 26

Hata hivyo Mariamu hakuelewa kazi ya Kristo. Simeoni ametabiri kwamba yeye ni nuru ya kuwaangaza mataifa; na malaika walitangaza kwamba kuzaliwa kwa Kristo kutawafurahisha mataifa. Mungu alikusudia kuwa yeye atakuwa Mwokozi wa ulimwengu. Lakini muda mrefu utapita bila watu kufahamu hivyo, hata mama wa Yesu pia. TVV 26.2

Mariamu hakuona ubatizo wa mateso, ambao Masihi mwenye kutawala kiti cha enzi cha Daudi atakaobatizwa. Katika maneno ya Simeoni kwa Mariamu: “Upanga utakuingia rohoni mwako pia.” Kwa rehema za Mungu, alimjulisha Mariamu, mama wa Yesu, matatizo ambayo ameanza kuyaona tayari. TVV 26.3

Simeoni alisema, “Tazama, mtoto huyu amewekwa ili kuwaangusha, na kuwainua wengi wa Israeli. Wataanguka na kuinuka tena. Hatuna budi kuanguka juu ya Mwamba wa kuvunjika kabla hatujainuliwa katika Kristo. Nafsi lazima kuondolewa kabisa. Wayahudi hawataipokea heshima itokanayo na unyenyekevu. Kwa hiyo hawatampokea Mwokozi. TVV 26.4

Kwamba mawazo ya wengi yapate kufunuliwa. Katika nuru ya maisha ya Mwokozi, watu wote, tangu Mwumbaji, hata mkuu wa giza wafunuliwe. Shetani amemtaja Mungu kuwa ni wa binafsi. Lakini kipawa cha kumtoa Kristo kilionyesha kuwa, ingawa Mungu huchukia dhambi, ni imara kuliko mauti. Kule kuchukua ukombozi wetu, Mungu hatazuia chochote mpaka ukombozi utimilike. Utajiri wote wa ulimwengu amenipa Kristo. Mungu husema, “Tumia utajiri wote, niliokupa ili kuwavutia watu wajue kuwa hakuna upendo mkuu kuliko huu niliowapeni. Furaha kamili itapatikana katika mimi tu. TVV 26.5