Go to full page →

Fundisho muhimu la utunzaji TVV 204

Baada ya kuwalisha makutano, byakula vingi vilibaki. Lakini Yesu alisema: “Kusanyeni mabaki, kitu kisipotee.” Kila kitu kinachoweza kumsaidia mtu mwenye njaa, kisitupwe bure. Pia pangekuwa na uangalifu katika mambo ya kiaroho. Watu wangetaka rafiki zao wa nyumbani washiriki kuala mikate hii iliyobarikiwa na yesu. Vivyo hivyo wale waliokuwa karamuni wangetaka rafiki zao waliokuwa nyumbani washiriki kula mkate ule ulioshuka kutoka mbinguni, ili kushibisha mioyo ya watu. Walikariri tena mambo waliyosikia, ambayo ni ya ajabu, ambayo ni maneno ya Mungu. Kitu kisipotee. TVV 204.2

Mwujiza wa mikate unafundisha fundisho la kumtegemea Mungu. Kristo alipowalisha watu 5,000 hakikuwepo chakula mkononi. Alikuwa msituni hapa, mahali pasipokuwa na chakula. Lakini alijua kuwa kundi hili la watu litachoka na kuona njaa, na yeye alikuwa pamoja nao, nao walihitaji chakula. Walikuwa mbali na miji yao, na wengine wao hawakuwa na fedha za kununulia chakula. Mungu alimweka Yesu mahali hapo, naye alimtegemea Baba yake wa mbinguni ili awasaidie na kuwapatia mahitaji yao. TVV 204.3

Sisi pia yatupasa kumtumaini Mungu. Hatuwezikuingia katika matatizo na kutumia ovyo uwezo Mungu aliotupatia. Lakini baada ya kufuata maongozi yake, tukapata kufika mahali sawa, tunaweza kutafuta msaada wake aliye na hekima na vitu vyote. Yeye ataangalia kila mtu aliye katika matatizo akijaribu kutunza njia ya Bwana. TVV 204.4