Go to full page →

Safari ya Usiku TVV 29

Ililazimika kusafiri wakati wa usiku ili kuona nyota, ambazo ndizo zinazowaongoza, lakini kila kituo wasafiri hao walichunguza jinsi unabii usemavyo. Walihakikishwa kuwa walikuwa wakiongozwa na Mungu. Safari yao ilikuwa ya furaha, ingawa ilikuwa ndefu. TVV 29.2

Walifika katika nchi ya Israeli, huko Yerusalemu, ndipo nyota ilitua juu ya hekalu. Basi waliharakisha kusonga mbele, wakiamini kuwa watasikia habari za kuzaliwa kwa Masihi zikizagaa pote. Lakini kwa mshangao wao, hawakuona hali yoyote ya kusisimua kwa ajili ya kuzaliwa kwa Masihi. TVV 29.3

Makuhani walikuwa wakishughulika na dini yao tu, huku wakiwatenga Wagiriki na Warumi, wakiwalaumu kuwa ni wenye dhambi. Mamajusi hawakuwa waabudu sanamu, lakini machoni pa Mungu walionekana kuwa wenye hali bora zaidi kuliko hao waliokuwa wakiitwa wenye dini, walakini walionekana kwa Wayahudi kama wakafiri. Maswali yao kuhusu kuzaliwa kwa Masihi hayakujibiwa. TVV 29.4