Go to full page →

Ushahidi wa kweli, kwamba Kristo alitoka kwa Mungu TVV 228

Kilichosababisha Wayahudi wamkatae Kristo ni ule uthibitisho wa tabia yake ya Uungu; na miujiza yake ambayo ilihusu msaada wa watu wenye dhiki. Maisha yake yalidhihirisha tabia ya Mungu, alifanya kazi ya mungu na kunena maneno ya Mungu, maisha ya jinsi hiyo mwujiza mkuu kuliko miujiza yote. TVV 228.1

Siku zetu hizi, watu wengi hupiga kelele na kusema, ‘Tuonyeshe ishara,’ au fanya miujiza sawa na watu wa kale, yaani Wayahudi. Kristo hatupi uwezo wa kujionyesha jinsi tulivyo, au kufanya mambo ya kuridhisha watu na kutufanya tujivune. Je, miujiza mikuu siyo ile ya kuvunja nguvu za Shetani zisitutawale? Uadui wetu na Shetani sio wa kuumbika, ila ni wa kuondoleka kwa neema ya Mungu. Mtu anayetawaliwa na hali ya upotovu, anapojitoa kwa Mungu hutawaliwa na hali ya unyofu, huo ni mwujiza umefanyika. Ndivyo ilivyo pia kwa mtu anayeishi katika hali ya udanganyifu, azindukapo na kuifahamu kweli. Mabadiliko ya moyo na kurekebika kwa tabia ya mtu ni mwujiza unaodhihirisha kuwa Mwokozi anaishi ndani yake. Katika kuhubiri neno la Mungu ishara inayodhihirika hapo ni kuwako kwa Roho Mtakatifu, ili kuotesha neno hilo na kulikuza; katika maisha ya walioliamini. TVV 228.2

Wale wanaotamani ishara kutoka kwa Yesu walikuwa wameshupaza mioyo yao. Walikuwa hawaoni kuwa kazi yake ilikuwa imetabiriwa na Biblia, na ilikuwa ikitimizwa. “Akawaambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.” Luka 16:31. TVV 228.3

Yesu akiwaacha wapinzani wake, aliingia mashuani pamoja na wanafunzi wake, wakavuka ziwa wakiwa na masikitiko makubwa. Walipofika ng’ambo, yesu alisema: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” Wayahudi wamefundisha kwamba chachu ni mfano wa dhambi. Katika kuondoka kwa ghafla kutoka Mgdala, wanafunzi walisahau kuchukua mikate. Walidhani kuwa Yesu alikuwa akiwaonya wasinunue mikate ya Mafarisayo, au Masadukayo. Hali yao ya upungufu wa kiroho ulikuwa ukiwafanya kila mara kutoelewa maana ya maneno ya Yesu. TVV 228.4

Sasa Yesu alithibitisha jinsi alivyowalisha watu maelfu kwa mikate michache na samaki wachache. Akawaambia kuwa hakumaanisha chakula cha mwili. Kulikuwa na hatari ya udanganyifu wa Mafarisayo na Masadukayo, ambao ungewadhuru wanafunzi katika imani yao. Wanafunzi walizidi kudhani kuwa Bwana wao angewapa ishara ya mbinguni kama ilivyotakiwa. Alikuwa na uwezo kufanya hivyo, na ishara hiyo ingewanyamazisha wabishi wake. Wanafunzi hawakufahamu unafiki wa wapinzani hao. Baada ya miezi mingi kupita, kristo alirudia kufundisha fundisho hilo. . . Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.” Luka 12:1 TVV 228.5