Go to full page →

Matatizo ya Yesu na jamaa yake TVV 43

Ndugu za Yesu walimwonea wivu, na wakaazimu kutokubaliana naye kwa vyo vyote. Hawakuelewa tabia vuke, Mabishano makubwa yalikuwako kati yao. Alikuwa Mwana wa Mungu, walakini alikuwa mtoto wa TVV 43.1

Ibinadamu tu. Kama mwumbaji, nchi ilikuwa katika uangalizi wake, walakini ufukara ulikuwa ndio maisha yake. Hakutafuta ukuu wa dunia hii, ila aliridhika tu na hali yoyote ya chini kabisa. Mambo haya yaliwachukiza ndugu zake. Hawakuridhika na hali yake ya unyofu, hata anapoonewa. Yesu hakueleweka kwa ndugu zake, kwa kuwa hakuwa kama wao. Kwa kutazama kwa watu, walikuwa kinyume cha Mungu, wala hawakumtegemea katika maisha yao. Mfano wa dini waliokuwa nao, haukuwatakasa kamwe. Tabia zao zilikuwa vile vile tu. Kielelezo cha Yesu, kwao kilikuwa chukizo la daima. Alichukia dhambi, na hakutaka kuona mambo maovu. Kwa kuwa maisha ya Yesu yalichukia dhambi, ndiyo sababu alipingwa. Uaminifu wa Yesu na hali yake isiyo na ubinafsi, vilikuwa dhihaka kwao. Uvumilivu wake na wema wake ulihesabiwa kama woga. TVV 43.2

Uchungu wote unaompata binadamu, hakuna sehemu ambayo haikumpata Yesu. Wengine walimdharau kwa ajili ya kuzaliwa mahali hafifu. Hata katika utoto wake alikabiliwa na mashutumu na dharau. Katika hayo yote, kama angejibu vibaya, kutenda vibaya, angeliangukia mbali, wala asingelikuwa kielelezo kamili kwa binadamu. Angelishindwa kutimiza mpango wa wokovu. Kama angelikubali dhambi hata ndogo mno, Shetani angalishangilia na ulimwengu ungalipotea. Kila mara aliyesabiwa kuwa mwoga, kwa ajili ya kutoshirikiana na ndugu zake, katika mambo maovu. Kila mara jibu lake lilikuwa, Imeandikwa, “Kumcha Bwana ndiyo hekima, na kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ Ayubu 28:28. Wengine walimfurahia, lakini wengi wao hawakumfurahia, maana maisha yake yalikuwa shutumu kwao, kwa vile alivyokuwa na hali ya unyofu kuliko yao. Vijana walimfurahia, lakini wengine hawakufurahia hali yake ya kutokubaliana nao kufanya mambo ya upuzi. Walipomtaka kwenda naye mahali pasipofaa, Yesu alijibu, Imeandikwa, “Kijana ataisafishaje njia yake? Kwa kulishika neno lake. . . Nimelishika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakutenda dhambi.” Zaburi 119:9, 11. TVV 43.3

Mara nyingi aliulizwa, “Kwa nini wewe u tofauti na sisi?” Alisema, Imeandikwa, ‘Heri wazitiio shuhuda zake. Naam, hawakutcnda ubatili, wamekwenda katika njia zake.” Zaburi 119:1, 2. TVV 43.4

Wakati alipoulizwa kuwa, kwa nini hujiungi na watoto wenzako wa Nazareti katika michezo, alisema: Imeandikwa “Nitajifurahisha sana kwa amri zako. Sitalisahau neno lako.” Zaburi 119:16. TVV 44.1

Yesu hakupigana, au kudai ili apatiwe haki yake. Hakulipa kisasi alipotendewa vibaya, ila alivumilia ujeuri huo tu. Mara nyingi aliulizwa kuwa, “Kwa nini unakubali ufedhuli unaofanyiwa hata na ndugu zako?” Alisema, Imeandikwa: “Mwanangu usisahau mafundisho yangu, shika amri zangu .... Rehema na kweli zisifarakane nawe. Zifunge shingoni mwako. Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, mbele za Mungu, na mbele za wanadamu.” Mithali 3:1-4. TVV 44.2