Go to full page →

Kutazamia Masihi wa Uongo TVV 15

Wayahudi hawakufahamu majilio na kazi ya Masihi. Hawakutafuta ukombozi kutoka dhambini, ila walitafuta kuokolewa na utawala wa Warumi. Walitazamia Masihi atakayewainua na kuwafanya kuwa taifa mashuhuri. Hivyo ndivyo njia iliandaliwa ya kumkataa Mwokozi. TVV 15.6

Wakati wa kuzaliwa kwa Kristo, taifa la Wayahudi lilikuwa mikononi mwa mabwana wageni, nao walikuwa wakihangaika katika mashindano ya ndani kwa ndani. Warumi waliowatawala, walimwongoa kuhani mkuu, na cheo chake kilishindaniwa kwa rushwa na mara kwa mara kwa mauaji. Hivyo kazi ya ukuhani ilizidi kuharibika zaidi na zaidi. Watu walikuwa katika hali ngumu ya ukorofi, huku wakitozwa kodi nzito na Warumi. Taifa zima lilikuwa katika msukosuko hasa, nchi ilijaa na kutokuridhika, choyo, uasi, ufedhuli. Kila mahali kulikuwa na hali ya ubariki kiroho. Katika giza lao na mateso yao, walitamani kuwa na mtu atakayewaondolea hali hiyo na kumsimamisha mfalme wa Israeli. Kwa hiyo waliutafsiri kufuatana na hali yao ya ubinadamu. TVV 16.1