Go to full page →

Kuponya kiroho kila mara hutangulia kuponya kimwili TVV 146

Leo watu maelfu huugua maradhi ya mwili kama yule mgonjwa kupooza, hutamani kupata ujumbe unaosema: “Dhambi zako zimesamehewa.” Dhambi ndiyo asili ya maradhi yao. Mponya wa roho peke yake ndiye awezaye kutia afya ya mwili. TVV 146.3

Yesu bado angali na uwezo wa kuponya kama alivyokuwa akiponya wagonjwa na kuwatangazia kusamehewa dhambi zao. “Yeye husamehe maovu yote.” “Hukuponya maradhi yote.” Zaburi 103:3; 1 Yohana 3:8; Yohana 1:4-10; 10:10; 1 Kor. 15:45. TVV 146.4

Kama vile mtu aliyeponywa alivyopita kati ya watu akibeba mzigo wake kama kwamba ni mzigo wa manyoya, watu walimpisha. Kwa mshangao mkubwa walinong’ onezana wakisema: “Leo umeona jambo jipya.” TVV 146.5

Mafarisayo walishangaa, wakawa kimya, wakashindwa la kusema, ila hawakukiri kuwa uwezo huo ni mkuu zaidi kuliko uwezo wa kibinadamu. Kutoka katika nyumba ya Petro, walikomwona mwenye kupooza akiponywa, walikwenda zao katika upotofu wao, wakitafuta njia ya kumnyamazisha Mwana wa Mungu. TVV 146.6

Nyumbani kwa yule aliyeponywa kulikuwa na shangwe kuu. Jamaa zake walimkusanyikia wakilia kwa furaha, wakishangaa wakidhani ni ndoto. Mwili uliokuwa umenyong’onyea sana ulikuwa safi kabisa. Alitembea sawasawa. Usafi na amani ilikuwa katika uso wake. Mtu huyu na jamaa yake walikuwa tayari kumwandama Yesu daima. Hakuna shaka yoyote iliyozima imani yao na nuru yao na kutia giza kamwe. TVV 146.7