Go to full page →

Kuifanya Kazi ya Mungu Kuwa Jambo la Kwanza KN 179

Je, si vizuri tukitumia likizo kwa mambo ya Mungu, tuwezapo kuamsha mafikara yetu na kukumbuka jinsi anavyotutendea? Je, halitakuwa jambo zuri kuifikiri mibaraka yake ya wakati uliopita, na kuyakumbuka maonyo ya ajabu yaliyotuingia nafsini mwetu hata tusiweze tena kumsahau Mungu? KN 179.5

Walimwengu wana sikukuu na likizo nyingi, na watu hushughulika na michezo, mashindano ya farasi, kucheza kamari, kuvuta tumbako, na ulevi. KN 180.1

Je, watu wa Mungu wasiwe na mikutano mitakatifu mara nyingi ambapo wanaweza kumshukuru Mungu kwa mibaraka yake mikubwa? KN 180.2

Twahitaji kanisani watu wenye uwezo kuleta katika mipango ya mambo na wenye kutoa kazi za kufaa kwa vijana wa kiume na wa kike za kupunguza mahitaji ya wanadamu na kutumikia wokovu wa roho za wanaume, wanawake, vijana, na watoto. Haitawezekana kwa wote kutoa wakati wao wote kwa kazi hii kwa sababu ya kazi ngumu wapaswayo kufanya kujipatia riziki zao za kila siku. Walakini hao nao wanazo likizo na sikukuu zao ambazo huweza kuzitumia kwa kazi ya Kikristo na kusaidia kwa njia hii, kama wasipoweza kutoa sehemu kubwa ya mali zao. KN 180.3

Ukipata likizo au sikukuu ifanye iwe siku nzuri ya furaha kwa watoto wako, pia ifanye siku ya kuwapendeza maskini na wenye taabu. Usiache siku hiyo ikapita bila kumletea Yesu shukrani na sadaka. KN 180.4