Go to full page →

Kutumia Vibaya Shuhuda Hizi KN 110

Idadi ya kwanza ya Shuhuda hizi iliyopata kuchapishwa ilikuwa na onyo juu ya kutumia isivyofaa nuru ambayo imetolewa hivi kwa watu wa Mungu. Nikasema kuwa wengine walikuwa wamefuata njia isiyo ya akili, waliposimulia imani yao kwa watu wasioamini, na uthibitisho ukawa umetakiwa, walikuwa wamesoma maandishi yangu badala ya kwenda kwenye Biblia kupata uthibitisho. Nalionyeshwa kuwa njia hii ilikuwa si sawa nayo ingeweza kuwachukiza vibaya wale wasioamini juu ya ukweli. Shuhuda hizi haziwezi kuwa na uzito ama maana kwa wale wasiojua lo lote rohoni mwao. Haifai kusoma habari zake kwa watu kama hao. KN 110.1

Maonyo mengine kwa habari ya matumizi ya Shuhuda hizi yametolewa mara kwa mara, kama ifuatavyo:“Wahubiri wengine wako nyuma sana. Wanadai kuusadiki ushuhuda uliotolewa na wengine wao hufanya madhara kwa kuzifanya utawala wa udhalimu kwa wale waliokuwa hawana ujuzi wo wote kwazo, hali hushindwa kuzifuata wao wenyewe. Wenyewe walipewa shuhuda mara kwa mara ambazo wamezidharau kabisa. Mwendo wa namna hii si sawa.” KN 110.2

“Naliona kuwa wengi wamefaidi kile Mungu alichoonyesha kwa habari ya dhambi na makosa ya wengine. Wameikaza mpaka imeelekea kuidhoofisha imani ya wengi katika mambo amoayo Mungu ameyaonyesha, na pia kulikatisha tamaa na kulivunja moyo kanisa.” 957 669, 670; KN 110.3