Go to full page →

Mwenendo Usiofaa KN 136

Kuchezacheza na mioyo ni uhalifu mkubwa machoni pa Mungu Mtakatifu. Lakini, wengine watawapendelea wasichana kutaka wapendane, kisha waende zao na kusahau kabisa maneno yote ambayo wamesema na matokeo yake ya baadaye. Uso mpya huwavuta, nao huyarudia maneno yale yale, wakimtolea mwingine mivuto ile ile. Tabia hii itadhihirika katika maisha ya unyumba. Ndoa siku zote haiuimarishi moyo wa kigeugeu, usiosimama imara, na kuwa na kanuni hasa. Huchoka na uamimfu, na mawazo mabaya yatadhihirika kwa matendo mabaya. Ni jambo muhimu kama nini, basi, kwamba vijana wayaweke tayari kabisa mawazo yao na kuulinda mwenendo wao hata Shetani asiweze kuwavuta kwa werevu kuiacha njia nyofu. KN 136.4

Mvulana apendaye maongezi na kujipatia urafiki wa msichana bila ya kujulikana na wazazi wa msichana hafanyi wajibu wa Mkristo bora kwa msichana huyo wala kwa wazazi wa huyu msichana. Kwa njia ya kupelekeana habari na kukutana kisirisiri aweza kujipatia mvuto wenye kuizidi akili ya huyo msichana, lakini kwa kufanya hivyo hadhihirishi ubora wala uadilifu wa roho ambayo kila mtoto wa Mungu atakuwa nao. Kusudi kupata mradi wao, wanafanya mambo yasiyo ya kweli wala yasiyo dhahiri, na ambayo hayapatani na Biblia, na kujidhihirisha kuwa waongo kwa wale wawapendao na kujaribu kuwa walezi waaminifu juu yao. Ndoa zinazoandikwa chini ya mivuto ya namna hii hazipatani na neno la Mungu. Mtu atakayempotosha binti fulani auacne wajibu umpasao, ambaye atamtia mashaka mawazoni mwake juu ya amri za Mungu zilizo dhahiri na halisi kuwatii na kuwaheshimu wazazi wake, si mtu atakayekuwa mwaminifu kwa mapatano ya ndoa. KN 137.1

“Usiibe” imeandikwa kwa chanda cha Mungu juu ya mbao za mawe, lakini, mara ngapi wizi wa hila wa upendo nufanywa na kutolewa udhuru! Uchumba wa kudanganyana hushikiliwa kupelekeana habari kisirisiri huendelezwa, mpaka upendo wa mtu asiye na maarifa, na kipimo kisichoko kwa wazazi wake na kilichoondolewa kutoka kwao na kuwekwa juu yake mwenyewe ambaye huonyesha kwa mwenendo huo huo anaofuata kuwa hastahili upendo wa huyo msichana. Biblia yakataza udanganyifu wa kila namna. Wenye kudai kuwa ni Wakristo, ambao maisha yao yameainishwa kwa uadilifu, na ambao huelekea kuwa wenye akili juu ya mambo yote mengine, hufanya makosa ya kutisha hapa. Huonyesha hali, na nia thabiti kuwa mawazo hayawezi kubadilika. Huvutwa sana na maoni na tamaa mbaya hata hawatamani kuichunguza Biblia na kushirikiana na Mungu. KN 137.2

Mojawapo ya Amri za Mungu inapovunjwa, hatua za kushuka katika hali ya chini hazina budi kuwepo. Mara visetiri vya stara ya kike vinapoondolewa uzinifu hauonekani kuwa jambo ovu mno. Ole, matokeo mabaya kama nini ya mvuto wa mwanamke kwa maovu huonekana ulimwenguni siku hizi! Kwa njia ya vishawishi (utongozi) wa “malaya” maelfu wanatiwa vifungoni gerezani, wengi hujiua, na wengi huyakatiza maisha ya watu wengine. Maneno haya ya Biblia, “Miguu yake inatelemkia mauti; hatua zake zinashikamana na kuzimu,” ni ya kweli kama nini. KN 137.3

Mioto mikubwa ya kuonya hatari imewekwa pande zote za njia ya maisha ili kuwazuia watu wasipakaribie manali pa hatari ambapo panakatazwa lakini hata, hivyo, wengi huchagua njia ya mauti, kinyume cha maonyo ya fikira, kwa kuidharau sheria ya Mungu, na kutojali kisasi cha Mungu. Wale ambao huihifadhi afya ya mwili, akili timamu, na tabia njema huzikimbia “tamaa za ujanani.” Wale ambao watajibidiisha kweli kweli kupinga uovu unaokiinua kichwa kigumu cha uovu, na cha kibun miongoni mwetu huchukiwa na kusengenywa na watenda mabaya wote, Iakini watatukuzwa na kutunzwa na Mungu. 1AH 41-51, 70-75. KN 138.1