Go to full page →

Ujumbe Waenea TK 233

Marekani ilikuwa kitovu cha harakati za ujio. Machapisho ya Miller na wenzi wake yalisambazwa hadi nchi za mbali, kila mahali palipokuwa na wamisionari ulimwenguni. Ujumbe wa Injili ya milele ulienea hadi mbali na kila mahali ukisema: “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” TK 233.3

Unabii uliokuwa unaonekana kuwa unatabiri kurudi kwa Kristo katika majira ya kuchipua ya mwaka 1844 ulikubalika na watu wengi. Wengi walisadiki kuwa hoja za vipindi vya unabii zilikuwa sahihi, nao waliacha kiburi cha kung’ang’ania maoni yao, waliupokea ukweli kwa furaha. Baadhi ya wachungaji waliacha mishahara yao namakanisa yao wakaungana kutangaza ujio Wakristo. Hata hivyo ni wachungaji wachache tu walioupokea ujumbe huu; hivyo kwa sehemu kubwa ulikabidhiwa kwa walei wanyenyekevu. Wakulima waliyaacha mashamba yao; mafundi waliziacha karakana zao;wafanyabiashara waliachana na bidhaa zao; watu wenye taaluma waliachana na nyadhifa zao. Walikabiliana kwa hiari na hali ngumu, kukosa mahitaji na mateso ili wawaite watu kuja kwenye toba na wokovu. Ujumbe wa ujio ulipokelewa na maelfu ya watu. TK 233.4