Go to full page →

Imani Yadumishwa TK 254

Roho wa Mungu bado alikuwa na wale ambao hawakuikana kwa pupa imani waliyokuwa wameipokea na kuzipinga harakati za Ujio. “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi y Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita- sita, rohoyangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.” Waebrania 10:35-39 TK 254.3

Mawaidha haya yametolewa kwa kanisa la siku za mwisho. Inaonekana wazi kwamba Bwana angeonekana kana kwamba anakawia. Watu wanaoambiwa hapa walikuwa wamefanya mapenzi ya Mungu katika kufuata uongozi wa Roho na Neno lake; lakini walikuwa hawalielewi kusudi lake katika mambo yaliyokuwa yamewapata. Walijaribiwa kuwa na mashaka kama Bwana alikuwa anawaongoza kweli. Wakati huo maneno haya yalikuwa mwafaka: “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Wakiwa wamenyong’nyea kwa matumaini yaliyovunjika, wasingeweza kusimama isipokuwa kwa imani juu ya Mungu na Neno lake. Kuikana imani yao pamoja na nguvu ya Roho Mtakatifu iliyokuwa imeambatana na ujumbe huo ingekuwa ni kurudi katika uharibifu. Njia pekee iliyokuwa salama kwao ilikuwa kushikilia nuru ambayo walikuwa wameipokea kutoka kwa Mungu, kuendelea kuyachunguza Maandiko, na kungoja kwa subira kupokea nuru zaidi. TK 255.1