Go to full page →

Mshahara wa Dhambi TK 332

“Mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” Wakati ambapo uzima ni urithi wa wenye haki, mauti ni fungu la waovu. “Mauti ya pili” ni kinyume cha uzima wa milele. Warumi 6:23; Ufunuo 20:14. TK 332.4

Kama matokeo ya dhambi ya Adamu, mauti imeifikia jamii yote ya wanadamu. Wote wanashushwa kaburini kwa namna ile ile. Na kwa kupitia mpango wa wokovu, wote watatolewa kutoka katika makaburi yao: kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.” TK 333.1

“Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.” Lakini kuna tofauti baina ya makundi mawili yatakayofufuliwa: “...watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”Matendo 24:15; 1 Wakorintho 15:22; Yohana 5:28, 29. TK 333.2