Go to full page →

Ushawishi wa Shetani kwa Wasomi TK 338

Kwa wenye elimu na waungwana, mkuu wa giza anaipeleka imani ya mizimu kwa kutumia mbinu makini na za kitaalamu zaidi. Anapendelea ubunifu wenye mandhari za kupendeza na mwonekano wenye ushawishi wa upendo na ukarimu. Anawaongoza wanadamu kujivunia sana hekima yao kiasi kwamba ndani ya mioyo yao wanamdhihaki Yule wa milele. TK 338.2

Shetani anawalaghai wanadamu sasa kama alivyowalaghai Adamu na Hawa pale Edeni kwa kuchochea shauku ya kujiinua nafsi. “mtakuwa kama Mungu” anatangaza, “mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:5. Imani ya mizimu inafundisha “kuwa mwanadamu ni kiumbe anayekua...kuelekea kwenye Uungu.” Na tena: “Hukumu itakuwa sahihi, kwa sababu ni hukumu ya nafsi...kiti cha enzi kipo ndani yako” Na mwingine anatangaza kuwa: “Kiumbe yeyote ambaye ni mwenye haki na mkamilifu ni Kristo.” TK 338.3

Shetani ameiweka asili ya dhambi ya mwanadamu mwenyewe kuwa ndiyo kanuni pekee ya uamuzi. Haya ni maendeleo ya kuelekea chini na siyo juu. Mwanadamu hataweza kwenda juu zaidi ya kiwango chake cha usafi na wema. Kama nafsi ndiyo kiwango chake cha juu kabisa, hataweza kufikia kiwango chochote cha juu zaidi. Neema ya Mungu pekee ina uwezo wa kumwinua mwanadamu. Akiachwa mwenyewe, mwelekeo wake lazima utakuwa ni wa kwenda chini. TK 338.4