Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Matokeo Yaliyopatwa katika Damu

    Baadala ya kudumisha watu wengi katika utii wa upofu kwa mafundisho yake, kazi ya Roma ikaishia katika kuwafanya makafiri na wapinduzi. Dini ya Roma wakaizarau kama ujanja wa wapadri. Mungu mmoja waliomujua ni mungu wa Roma. Waliangalia tamaa yake na ukatili kama tunda la Biblia, na hawakutaka tena kusikia habari yake.TSHM 132.1

    Roma ilieleza vibaya tabia ya Mungu, na sasa watu wakakataa vyote viwili Biblia na Muumba wake. Katika urejeo, Voltaire na wafuasi wake wakakataa kabisa Neno la Mungu yote pamoja kutawanya kukana Mungu. Roma ikakanyaga watu chini ya kisigino chake cha chuma; na sasa watu wengi wakatupia mbali kuzuiwa kote (amri). Walipokasirishwa, wakakataa kweli na uongo pamoja.TSHM 132.2

    Kwa kufunguliwa kwa Mapinduzi, kwa ukubali wa mfalme, watu wakapata kwa mitaa ya kawaida mfano wa juu kuliko ule wa wakuu na mapadri pamoja. Kwa hivyo kipimo cha uwezo kulikuwa katika mikono yao; lakini hawakutayarishwa kukitumia kwa hekima na utaratibu (kiasi). Watu waliotendewa vibaya wakakusudia kulipiza kisasi wao wenyewe. Walioonewa wakatumia fundisho walilojifunza chini ya uonevu na wakawa watesi wa wale waliowatesa.TSHM 132.3

    Ufransa ukavuna katika damu mavuno ya utii wake kwa Roma. Mahali Ufransa, chini ya Kanisa la Roma, uliweka tita (kigingi) la kwanza kwa mwanzo wa Matengenezo, hapo Mapinduzi yakaweka mashini yake ya kukata watu vichwa ya kwanza. Ni mahali pale ambapo, kwa karne ya kumi na sita, wafia dini wa kwanza wa imani ya Kiprotestanti walichomwa, watu wa kwanza walikatwa vichwa kwa karne ya kumi na mnani. Wakati amri za sheria ya Mungu ziliwekwa pembeni, taifa likaingia katika giza na machafuko ya mambo ya utawala. Vita juu ya Biblia katika historia ya ulimwengu ikajulikana kwa jina la Utawala wa hofu kuu. Yeye aliyeshinda leo akahukumiwa kesho yake.TSHM 132.4

    Mfalme, waongozi wa dini, na wakuu wakalazimishwa kujiweka chini ya mambo ya mabaya ya watu wenye wazimu. Wale walioamuru kifo cha mfalme mara wakamfuata kwa jukwaa. Machinjo makubwa ya wote waliozaniwa kuwa na uchuki kwa Mapinduzi yakakusudiwa. Ufransa ukawa shamba kubwa la mabishano, yaliyowayawaya kwa hasira kali ya tamaa. “Katika Paris,fujo ikafuata fujo ingine, na wakaaji wakajitenga katika machafuko ya fitina, yaliyoonekana yenye bidii si kwa kitu kingine bali kusudi moja. ... Inchi ilikuwa karibu kushindwa, majeshi yalikuwa yakifanya fujo kwa ajili ya deni ya malipo, wakaaji wa Paris walikuwa na njaa, mitaa ikaangamizwa na wanyanganyi, na utamaduni na maendeleo vilikuwa karibu kukomeshwa katika machafuko ya mambo ya utawala na upotovu.”TSHM 132.5

    Kwa yote haya watu wakajifunza mafundisho ya ukali na mateso ambayo Roma ilifundisha kwa nguvu sana. Haikuwa sasa wanafunzi wa Yesu waliokokotwa kwa kigingi. Ni Zamani walikuwa ao kuchinjwa wala kulazimishwa kujihamisha. “Damu ya wapadri ilitiririka juu ya majukwaa. Majahazi na gereza, zamani zilikuwa zikijaa na Wahuguenots, yakajaa sasa na watesi wao. Wakafungiwa na minyororo kwa viti vyao na kukokota kwa gasia, wapadri wa Katoliki wa Roma wakajua misiba ile yote ambayo kanisa lao lilipatisha kwa bure kabisa juu ya wazushi wapole.” (Tazama Nyongezo.)TSHM 133.1

    “Ndipo siku zile zikaja ... wakati wapelelezi walijificha kwa kila pembe; wakati mashine ya kukatia vichwa ilikuwa ndefu na ya nguvu kwa kazi kila asubuhi: wakati magereza zikijaa kama kiwanja kama chumba cha chini cha merikebu ya watumwa; wakati damu na uchafu vikawa kama pofu na kutiririka katika mifereji ya mabati hata mto seine” ... mistari mirefu ya watumwa yalisukumwa chini kwa marisaa makubwa. Matundu yalifanywa katika upande wa chini wa mashua kubwa iliosongana. ... Hesabu ya vijana wanaume na wanawake wa miaka kumi na saba waliuawa kwa serekali ile mbaya sana, inajulikana kuwa mamia. Watoto wachanga waliotengwa kwa kifua cha mama wakarushwa kutoka kwa mkuki na kwa mkuki mwengine kwa cheo cha wa Jacobins.” (Tazama Nyongezo.)TSHM 133.2

    Haya yote yalikuwa ni mapenzi ya Shetani. Amri yake ni madanganyo na makusudi yake ni kuleta uharibifu juu ya watu, kutia haya kiumbe cha Mungu, kwa kuharibu kusudi la Mungu la upendo, na kwa hiyo kuleta sikitiko mbinguni. Basi kwa mambo yake ya ufundi ya kudanganya, huongoza watu kutupa laumu juu ya Mungu, kana kwamba mateso haya yote yalikuwa matokeo ya shauri la Muumba. Wakati watu waliona dini ya Roma kuwa danganyifu, akawashurutisha kuzania dini yote kama danganyifu na Biblia kama hadisi (uongo).TSHM 133.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents