Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  35 / UHURU WA ZAMIRI UNATISHWA

  Kanisa la Roma sasa linapendelewa sana na Waprotestanti kuliko miaka ya zamani. Katika inchi hizo ambamo Kanisa la Kikatoliki linapata mwendo wa kuunganisha kwa kupata mvuto, mawazo yanaanza kusimamiwa ya kwamba hakuna tofauti sana juu ya mambo ya lazima kama ilivyozaniwa na ya kwamba ukubali ule mdogo kwa upande wetu utatuongoza katika mapatano bora pamoja na Roma. Kulikuwa wakati Waprotestanti walifundisha watoto wao ya kwamba kutafuta umoja na Roma kungekuwa kutokuwa na uaminifu kwa Mungu. Lakini ni tofauti kubwa ya namna gani tunaona katika taarifa ya sasa!TSHM 275.1

  Watetezi wa dini ya Rome (Papa) wanatangaza kwamba kanisa limeshitakiwa uwongo, ya kwamba si haki kuhukumu kanisa la leo kwa utawala wake wa mda wa karne nyingi za ujinga na giza. Wanarehemu ukali wake wakuogopesha kwa ushenzi wa nyakati zile.TSHM 275.2

  Je, watu hawa hawakusahau madai ya kutoweza kukosa kulikowekwa na uwezo huu? Roma inadai ya kwamba “kanisa halikukosa kamwe; wala kukosa kwa wakati ujao, kufuatana na Maandiko, halitakosa daima.”TSHM 275.3

  Kanisa la Roma halitaacha kamwe madai yake kwa kutoweza kukosa (infallibilité). Acha vizuizi (amri) vilivyoamriwa sasa na serikali za dunia vitoshwe na Roma irudishwe katika mamlaka yake ya kwanza, na hapo kwa upesi ingekuwa uamsho wa uonevu wake na mateso.TSHM 275.4

  Ni kweli ya kwamba Wakristo wa kweli wanakuwako katika ushirika wa kanisa la Kikatoliki la Roma. Maelfu katika kanisa lile wanamtumikia Mungu kufuatana na nuru bora wanayokuwa nayo. Mungu anatazama na upendo wa huruma juu ya nafsi hizi, zilizolelewa katika imani ile ya kudanganya na isiyotosheleka. Ataleta mishale ya nuru kupenya giza, na wengi watakamata misimamo yao pamoja na watu wake.TSHM 275.5

  Lakini Kanisa la Roma kama chama haliko tena katika umoja na habari njema ya Kristo sasa kuliko kwa wakati wa kwanza. Kanisa la Roma linatumia shauri lo lote kwa kupata utawala wa ulimwengu, kuanzisha tena mateso, na kuharibu mambo yote ambayo Waprotestanti wamefanya. Kanisa la Kikatoliki liko linapata nafasi kwa pande zote. Angalia kuongezeka kwa makanisa yake. Tazama uwingi wa vyuo vyao vikubwa (colleges) na seminaires, vinavyosimamiwa na Waprotestanti. Tazama usitawi wa utaratibu wa sala katika Uingereza na maasi ya mara kwa mara kwa vyuo vya Wakatoliki.TSHM 275.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents