Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Usalama huko Wartburg

  Katika salama ya urafiki wa Wartburg, Luther akafurahi kuwa inje ya fujo ya vita. Lakini kwa sababu ni mtu aliyezoea maisha ya kazi na magumu makali, hangevumilia kukaa bila kufanya lolote. Wakati wa siku za upekee, hali ya kanisa ikafika kwa mawazo yake. Akaogopa kuzaniwa kuwa mwoga kwa kujitosha kwa mabishano. Ndipo akajilaumu mwenyewe kwa uvivu wake na kujihurumia mwenyewe.TSHM 77.3

  Lakini, kila siku alifanya kazi ya ajabu kuliko ingeonekana mtu mmoja kuweza kufanya. Kalamu yake haikukaa bure. Adui zake walishangaa na kufazaika kwa ushuhuda wazi kwamba alikuwa angali akitumika. Kwa wingi wa vitabu vidogo vya kalamu yake vikaenea katika Ujeremani pote. Akatafsiri pia Agano Jipya kwa lugha ya Ujeremani. Kutoka kwa mwamba wake wa Patemo, akaendelea kwa mda karibu mwaka mzima kutangaza injili na kukemea makosa ya nyakati. Mungu akavuta mtumishi wake kutoka kwa jukwaa ya maisha ya watu. Katika upekee na giza ya kimbilio lake mlimani, Luther akatengwa kwa misaada ya kidunia na kukosa sifa ya kibinadamu. Aliokolewa basi kwa kiburi na kujitumainia vinavyoletwa mara nyingi na ushindi.TSHM 77.4

  Namna watu wanavyofurahia kwa uhuru ambao kweli inawaletea, Shetani anatafuta upotosha mawazo yao na upendo kutoka kwa Mungu na kuwaimarisha kwa wajumbe wa kibinadamu, kuheshimu chombo na kutojali Mkono ambao unaoongoza mambo ya Mungu. Mara nyingi waongozi wa dini wanaposifiwa huongozwa kujitumainia wenyewe. Watu wanakuwa tayarikuwaangalia juu ya uongozi badala ya Neno la Mungu. Kutoka katika hatari hii Mungu alitaka kulinda Matengenezo. Macho ya watu yalimugeukia Luther kama mfasi wa ukweli; aliondolewa ili macho yale yote yapate kuongozwa kwa Mwenyezi wa milele wa ukweli.TSHM 77.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents