Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Berquin Shujaa

    Lakini juhudi ya Berquin ikazidi kuwa na nguvu. Akakusudia mpango wa nguvu zaidi. Hakusimama tu kwa kutetea ukweli, lakini akashambulia kosa. Adui zake waliokuwa na juhudi na ukaidi zaidi walikuwa watawa wenye elimu kutoka kwa idara ya elimu ya tabia na sifa za Mungu na dini (theologie) katika chuo kikubwa (universite) cha Paris, mojawapo ya mamlaka ya kanisa ya juu sana katika taifa. Kwa maandiko ya waalimu hawa, Berquin akapata makusudi kumi na mbili ambayo akaitangaza wazi wazi kuwa kinyume cha Biblia,” na akauliza mfalme kujifanya muamzi katika shindano.TSHM 99.4

    Mfalme, kwa kuwa na furaha ya nafasi ya kushusha majivuno ya hawa watawa wenye kiburi, akaalika wakatoliki kutetea jambo lao kwa kufuata Biblia. Silaha hii haingewasaidia zaidi; mateso na kifo cha mtu wa kuchoma ilikuwa ndizo silaha ambazo walizifahamu zaidi namna ya kutawala. Sasa wakajiona wenyewe kuanguka katika shimo walilotumaini kumtumbukiza Berquin. Wakatafuta wenyewe namna gani ya kujiepusha.TSHM 99.5

    “Kwa wakati ule wakaona kando ya mojawapo ya njia sanamu ya bikira iliyovunjwa.” Makundi yakakusanyika mahali pale, wakilia na hasira. Mfalme akachomwa moyo sana . “Haya ndiyo matunda ya mafundisho ya Berquin,” watawa wakapaza sauti. “Kila kitu ni karibu kugeuzwa--dini, sheria, kiti cha ufalme chenyewe kwa mapatano hii ya Luther.”TSHM 100.1

    Mfalme akatoka Paris, na watawa wakaachiwa huru kufanya mapenzi yao. Berquin akahukumiwa na kuhukumiwa kifo. Kwa hofu kwamba Francis angetetea tena kwa kumwokoa, hukumu ikafanyika kwa siku ile ile ilio tamkwa. Kwa sasa sita za mchana msongano wengi ukakusanyika kwa kushuhudia jambo hili, na wengi wakaona kwa mshangao kwamba mtu aliyeteswa alichaguliwa miongoni mwa watu bora na wahodari zaidi wa jamaa bora za Ufransa. Mshangao, hasira, zarau, na uchuki wa uchungu yakahuzunisha nyuso za kundi lile, lakini kwa uso mmoja haukuwa na kivuli. Mfia dini alikuwa na zamiri tu ya kuwako kwa Bwana wake.TSHM 100.2

    Uso wa Berquin ulikuwa ukingaa na nuru ya mbinguni. Alivaa vazi kama joho laini la kungaa, chuma puani na soksi ya zahabu.” Alikuwa karibu kushuhudia imani yake mbele ya Mfalme wa wafalme, na hakuna dalili iliyopasa kusingizia furaha yake.TSHM 100.3

    Wakati mwandamano ulipokuwa ukisogea polepole katika njia zilizosongana, watu wakapatwa na mshangazo wa ushindi wa furaha wa uvumilivu wake. “Yeye anakuwa,” wakasema, “kama mmoja anayekaa katika hekalu, na akifikiri vitu vitakatifu.”TSHM 100.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents