Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uovu Mbaya Sana Kupita Mengine

    Lakini uovu mbaya zaidi miongoni mwa matendo maovu ya karne za kutisha ilikuwa machinjo ao mauaji matakatiifu ya SaintBartheiemy. Chini ya mkazo wa mapadri na maaskofu, mfalme wa Ufransa akatoa ukubali wake. Kengele kulia katika ukimya wa usiku, ikatoa ishara ya mauaji. Maelfu ya Waprotestanti, walipokuwa wakilala nyumbani mwao, wakitumaini neno la heshima la mfalme wao, wakakokotwa na kuuawa.TSHM 127.2

    Machinjo yakaendelea kwa siku saba katika Paris. Kwa agizo la mfalme mauaji yakaenea kwa miji yote mahali Waprotestanti walikuwako. Wakuu na wakulima, wazee na vijana, wamama na watoto, wakachinjwa pamoja. Katika Ufransa po pote kulikuwa nafsi 70.000 za ua la taifa wakauawa.TSHM 127.3

    “Wakati habari ya mauaji ilipofika Roma, furaha ya mapadri haikujua mpaka. Askofu wa Lorraine akatolea mjumbe zawadi ya mataji elfu; mzinga wa Saint-Ange mtakatifu akapiga ngurumo ya salamu za furaha; na kengele zikalia kwa minara ya makanisa yote; mioto ya furaha ikageuza usiku kuwa mchana; na Papa Gregoire XIII, pamoja na maaskofu na wakuu wengine wa kanisa, wakaenda kwa mwandamano mrefu kwa kanisa la Saint-Louis, mahali askofu wa Lorraine aliimba Te Deum. ... Nishani ikapigwa kwa kumbukumbu la machinjo. ... Padri wa Ufransa ... akasema kwa ajili ya`siku ile akijaa na kicheko na furaha, wakati baba mtakatifu alipokea habari, na akaenda kwa hali ya heshima kwa kumshukuru Mungu na Mtakatifu Ludoviko.”TSHM 127.4

    Roho mbaya ya namna moja iliyosukuma kuuawa kwa SaintBarthelemy akaongoza pia katika maonyesho za Mapinduzi. Yesu Kristo akatangazwa kuwa kama mjanja, na kilio cha makafiri wa Ufransa kikawaangamiza wamaskini,” maana yake Kristo. Matukano na uovu yakaenda pamoja. Katika haya yote, ibada ilitolewa kwa Shetani, wakati Kristo, katika tabia zake za kweli, usafi, na upendo wake wa kupendelea wengine kuliko yeye mwenyewe, alisuubiwa.”TSHM 128.1

    “Yule nyama anayetoka katika shimo pasipo mwisho atafanya vita nao; naye atawashinda na kuwaua.” Ufunuo 11:7. Mamlaka ya kukana kumjua Mungu iliyotawala katika Ufransa wakati wa Mapinduzi na utawala wa Hofu kuu ilipigana vita ya namna hiyo kumpinga Mungu na Neno lake. Ibada ya Mungu ikakomeshwa na baraza la Taifa. Vitabu vya Biblia vikakusanywa na kuchomwa mbele ya watu wote. Vyama vya Biblia vikaharibiwa. Siku ya kustarehe ya juma ikakatazwa, na mahali pake kila siku kumi ikatengwa kwa makutano. Ubatizo na ushirika Mtakatifu (Meza ya Bwana) vikakatazwa. Matangazo yakawekwa kwa mahali pa maziko kutangaza kwamba mauti ni usingizi wa milele.TSHM 128.2

    Ibada ya dini yote ikakatazwa, ila tu ile ya uhuru na ya inchi. “Askofu wa kushika sheria wa Paris akaletwa ... kwa kutangaza kwa mapatano kwamba dini aliyofundisha kwa miaka nyingi ilikuwa, katika heshima yote, sehemu ya ujanja wa mapadri, ambayo haikuwa na msingi hata katika historia ao ukweli takatifu. Katika maneno ya kutisha sana na ya wazi, akakana kuwako kwake Mungu ambako alijitakasa kwa ajili yake.”TSHM 128.3

    “Nao wanaokaa juu ya dunia watafurahi juu yao na kuwachekelea. Watapelekeana zawadi moja kwa wengine, kwa sababu manabii hawa wawili waliwatesa wao wanaokaa juu ya dunia.” Ufunuo 11:10. Ufransa kafiri ukanyamazisha sauti yenye kulaumu ya washahidi wawili wa Mungu. Neno la ukweli likalala chini kama maiti” katika njia zake, na wale waliochukia sheria za Mungu wakafurahi. Watu kwa wazi wakachafua Mfalme wa mbinguni.TSHM 128.4

    Te Deum : Wimbo wa kushukuru wa kanisa la kikatoliki unaoanza na maneno haya : ‘’Bwana tunakusifu”.TSHM 128.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents