Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Vyama vya Wafanyakazi na Amana, Sura ya 174

  Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Yakobo 5:7.Mar 182.1

  Vyama vya wafanyakazi vitakuwa moja ya mawakala ambao watailetea dunia wakati wa taabu kiasi ambacho hakijawahi kuwepo tangu ulimwengu kuumbwa.Mar 182.2

  Katika majiji yetu makuu yote mashirikisho na vyama vitawafunga watu katika mafungu. Watu watawatawala wengine na kuwataka kutenda mengi. Maisha ya wale watakaokataa kuungana na vyama hivi, yatakuwa hatarini.Mar 182.3

  Kazi ya watu wa Mungu ni kufanya maandalizi kwa ajili ya wakati ujao, ambao utakuja kwao kwa nguvu inayopofusha. Duniani ukiritimba mkubwa utaundwa. Watu watajifunga wenyewe pamoja katika vyama ambavyo vitawafunga katika mafundo ya adui. Watu wachache wataungana ili kukamata njia zote ziwezazo kupatikana katika biashara husika. Vyama vya kibiashara vitaundwa, na wale watakaokataa kujiunga na vyama hivi watatambulika. . .Mar 182.4

  Vyama hivi ni moja ya ishara za siku za mwisho. Watu wanafungwa katika mafungu tayari kwa ajili ya kuchomwa moto. Hawa wanaweza wakawa ni washiriki wa kanisa, lakini kama wanahusika na vyama hivi, hawawezi kushika amri za Mungu; kwani kuwa mwanachama wa vyama hivi ni kupuuza amri kumi za Mungu.Mar 182.5

  “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.”. . . Je, watu wanawezaje kutii maneno haya, na kulinda miunganiko hii ambayo itawanyang’anya daraja la maskini faida zilizo zao, kwa kuwazuia kununua au kuuza, isipokuwa wametimiza masharti fulani ?Mar 182.6

  Wale wanaodai kuwa watoto wa Mungu hawapaswi kwa namna yoyote kufungamana na vyama vya ushirika ambavyo vinaundwa sasa na vitakavyoundwa. Bwana analipiga marufuku hili. Je, wale wanaojifunza unabii, hawawezi kuona na kuelewa kilicho mbele yetu?Mar 182.7

  Masuala ya muhimu sharti yazingatiwe, hebu na tutamani kufichwa ndani ya ufa wa mwamba, ili tupate kumwona Yesu, na kuhuishwa na Roho wake Mtakatifu. Hatuna muda wa kupoteza, hata kidogo.Mar 182.8

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents