Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Marufuku Kununua au Kuuza, Sura ya 175

  Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Ufunuo 13:17.Mar 183.1

  Wakati unakuja ambapo hatutauza katika bei yoyote ile. Si muda mrefu tamko litatolewa la kupiga marufuku mtu kununua au kuuza isipokuwa wale tu wenye alama ya mnyama.Mar 183.2

  Katika pambano kuu la vita vya mwisho dhidi ya Shetani wale walio watiifu kwa Mungu watashuhudia kila riziki ya kidunia ikiondolewa. Kwa sababu watakataa kuvunja sheria yake ili kutii mamlaka ya kidunia, watakatazwa kununua au kuuza.Mar 183.3

  Mamlaka za kidini, zinazojifungamanisha na mbingu kwa uweledi, wakidai kuwa na tabia ya mwana-kondoo, wataonesha kwa matendo yao ya kwamba wana moyo wa joka na kwamba wanachochewa na kutawaliwa na Shetani. Muda unakuja wakati watu wa Mungu watakapohisi mkono wa mateso kwa sababu wanaishika siku ya saba kama takatifu.Mar 183.4

  Wakati unakuja ambapo wale wazishikao amri hawataweza kununua au kuuza. Harakisha kuchimbua talanta zako zilizozikwa. Kama Mungu amekukirimia fedha, jioneshe mwenyewe kuwa mwaminifu katika hicho ambacho umeaminiwa; fungua kitambaa chako, kisha uweke talanta zako katika matumizi yaliyokusudiwa, ili Kristo ajapo, apokee kilicho chake pamoja na riba. Wakati wa mwisho wa yote, kabla ya kufungwa kwa kazi hii, maelfu watawekwa katika madhabahu. Wanaume kwa wanawake wataiona kuwa fursa yenye baraka kushiriki kazi ya kuandaa roho tayari kusimama katika siku ile kuu ya Mungu, na watakuwa tayari kutoa maelfu ya fedha kuliko wavyotoa leo. Kama upendo wa Kristo ungekuwa unawaka mioyoni mwa wale wanaojiita kuwa watu wake, tungeona roho hiyo hiyo ikidhihirishwa leo. Kama wangetambua jinsi mwisho wa kazi yote ya wokovu wa roho za watu ulivyo karibu, wangejinyima walivyo navyo kwa uhuru kama walivyofanya washiriki wa kanisa la awali. Wangetenda kazi kwa ajili ya kuendeleza mpango wa Mungu kwa bidii kama jinsi walimwengu wanavyofanya kazi ili kujikusanyia mali. Busara na ustadi vingetumiwa hapa, na bidii na kufanya kazi kusiko na ubinafsi kungeonekana katika kukusanya mahitaji, siyo kwa ajili ya kulimbikiza, bali kwa ajili ya kumimina katika hazina ya Bwana.Mar 183.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents