Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uprotestanti Kuunganika na Upapa, Sura ya 179

  Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. Ufunuo 17:12,13.Mar 187.1

  Tunapokaribia zahama ya mwisho, huu ni wasaa wa muhimu sana wa kuhakikisha kwamba kunakuwepo na mapatano na umoja kati ya watendaji wa Bwana. Ulimwengu umejazwa na dhoruba na vita na utofauti. Hata hivyo, chini ya kiongozi mmoja - mamlaka ya upapa - watu wataungana ili kumpinga Mungu kwa njia ya kuwapinga mashahidi wake.Mar 187.2

  Ni mamlaka ipi itoayo ufalme wake kwa mamlaka hii ya Kirumi? Uprotestanti, mamlaka ambayo, hata ingawa inadai kuwa na tabia na roho ya Mwana-Kondoo na kufungamana na Mbingu, inanena kwa sauti ya joka. Inaongozwa na mamlaka inayotoka chini.Mar 187.3

  “Hawa wana shauri moja.” Pote kutakuwa na muunganiko wa umoja, mwafaka mkubwa, shirikisho la majeshi ya Shetani. “nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.” Kwa namna hiyo inadhihirishwa mamlaka isiyo na mantiki, yenye kukandamiza uhuru wa dini, uhuru wa kumwabudu Mungu kulingana na matashi ya dhamiri, kama iIivyodhihirika kupitia kwa upapa, wakati ule ulipotesa wale waliodiriki kukataa kufuata kanuni za kidini na ibada za Kirumi.Mar 187.4

  Katika vita vitakavyokuwepo siku za mwisho mamlaka zote zilizo potofu ambazo zimeasi na hivyo kutotii sheria ya Yehova, zitaungana katika kupinga watu wa Mungu. Katika vita hivi, Sabato ya amri ya nne itakuwa suala kuu; kwani katika amri ya Sabato mtoaji mkuu wa sheria anajitambulisha mwenyewe kama Mwumbaji wa mbingu na nchi.Mar 187.5

  Kupitia katika makosa mawili makuu, dhana ya roho kutokufa na utakatifu wa Jumapili, shetani atawavuta na kuwaweka watu chini ya udanganyifu wake. Wakati hiyo dhana ya roho kutokufa inaweka msingi wa umizimu, hilo la pili la utakatifu wa Jumapili, linafanya muunganiko wa kihisia na Rumi. Waprotestanti wa Marekani watakuwa mbele kabisa kunyoosha mikono yao hadi ng’ambo ya ghuba ili kukamata mkono wa umizimu; mikono yao itapita juu ya lile rima kuu ili kushikana na mamlaka ya Kirumi; na mvuto wa umoja wa hawa watatu, nchi hii itafuata nyayo za Rumi katika kukanyaga haki za dhamiri za watu.Mar 187.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents