Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Njia Bora na ya Kiungwana Zaidi, Sura ya 18

    Jiosheni, jitakaseni; ondocni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni Walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane Isaya 1:16,17.Mar 26.1

    Ujinga, kupenda starehe, na mazoea ya dhambi, uchafu wa moyo, mwili, na roho, vinaufanya ulimwengu kuwa na ukoma wa kimaadili; malaria ya kimaadili inayofisha inangamiza maelfu kwa makumi elfu.Mar 26.2

    Wengi wamezama katika dhambi. Wengi wanafadhaika Wamejawa na mateso, shida, kutoamini, na kukata tamaa. Magonjwa ya kila aina ya kimwili na kiroho yanawasibu. Wanatamani wapate faraja dhidi ya mateso yao, na Shetani anawashawishi kutafuta faraja hiyo katika tamaa na anasa ambazo huwasababishia uharibifu na kifo. Anawapatia tunda la Sodoma, ambalo litakuwa majivu katika vinywa vyao.Mar 26.3

    Taswira ya kutisha ya ulimwengu imeoneshwa mbele yangu. Kuporomoka kwa maadili kumeenea kila mahali. Ufuska ni dhambi maalum ya kila kizazi. Uhalifu na uovu haujawahi kushamiri kama ulivyo sasa.... Uovu unaoongezeka hauko kwa wasioamini na wenye dhihaka tu. Bora ingekuwa hivyo. Lakini sasa siyo hivyo. Watu wengi wanaojidai kuwa na dini ya Kristo wana hatia. Hata baadhi ya wale wanaojidai kutazamia kuonekana kwake hawako tayari kwa tukio hilo kama vile Shetani usivyokuwa tayari. Hawajitakasi na uchafu wote. Wametumikia tamaa zao kwa muda mrefu kiasi kwamba imekuwa kawaida kwa mawazo yao kuwa machafu na fikra zao kuwa batili. Haiwezekani kuzifanya akili zao ziwaze mambo yaliyo safi na matakatifu kama isivyokuwa rahisi kuyafanya maji ya mto Niagara yapande mlima. . . Kila Mkristo atapaswa kujifunza kudhibiti tamaa zake na kutawaliwa na kanuni. . .Mar 26.4

    Kama ufuska, uchafu, uzinzi, uhalifu, na mauaji yamekuwa mambo ya kawaida miongoni mwa wale wasioujua ukweli, na wasiotaka kuongozwa na na kanuni za neno la Mungu, basi ni muhimu zaidi kwa kundi lile wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo, washirika wa Mungu pamoja na malaika, kuwaonesha njia iliyo bora na ya kuingwana zaidi! Usafi na uadilifu wao ni muhimu uonekane wazi kwamba wako tofauti na wale wanaoongozwa na tamaa mbaya!Mar 26.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents