Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushuhudiaji wa Mtu kwa Mtu, Sura ya 97

    Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, hali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16Mar 105.1

    Je, kwa nini wote wanaodai kumpenda Mungu hawatafuti namna ya kuwaangazia majirani na washirika wao, ili wasiendelee kudharau wokovu huu mkuu? Kristo alijitoa ili afe kifo cha aibu na chenye maumivu makali, roho yake ikipitia taabu kuu kwa ajili ya kuokoa roho zinazoangamia. Naam! Kristo anao uwezo, na yupo tayari, tena ni shauku yake, kuokoa wote watakaomjia!Mar 105.2

    Ongea na roho zilizo katika hatari na zielekeze kumtazama Yesu msalabani, akifa kwa makusudi ya kumfanya aweze kusamehe. Nena na mwenye dhambi moyo wako ukiwa umejaa wema na upendo wa Yesu wenye huruma. Hebu nena kwa dhati kabisa; lakini Iisisikike hata neno moja la ukali au kutoka toka kwa yule anayejaribu kuiongoa roho akiielekeza kumtazama Yesu kwa ajili ya uhai. Kwanza kabisa, iweke roho yako wakfu kwa Mungu. Unapoendelea kumtazama Mpatanishi wetu aliyeko mbinguni, moyo wako utavunjika. Baada ya hapo, ukiwa na moyo uliolainishwa na kunyenyekezwa, unaweza kuelekeza wadhambi wanaotubu sasa ukiwa na ufahamu fika wa uwezo wa upendo unaookoa. Hebu sali na watu hawa, ukiwaleta kwa imani chini ya msalaba; unganisha mawazo yao na yako, na kaza jicho la imani pale unapopaswa, pale kwa Yesu, abebaye dhambi zote. Ukiweza kuwaelekeza waache kutazama umaskini wao, na nafsi zao zenye dhambi na badala yake wamtazame Mwokozi, ushindi utakuwa umepatikana. Wao wenyewe, watamtazama Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu. Wataona Njia, Kweli na Uzima. Jua la Haki litang’aza miali yake angavu mioyoni. Mkondo wenye nguvu wa upendo unaokomboa utamiminika katika roho iliyojeruhiwa na yenye kiu, na mwenye dhambi ataokolewa na Yesu Kristo.Mar 105.3

    Kristo aliyesulubiwa — liwe gumzo lako na wimbo wako, na utaona jinsi hilo linavyoongoa roho. Huu ni uwezo na hekima ya Mungu inayokusanya roho kwa Kristo. Kauli zilizo rasmi sana, tungo zilizowekwa tayari kwa namna fulani na uwasilishaji wa masomo yaletayo ubishani tu, matokeo yake si mazuri sana. Upendo wa Mungu unaoyeyusha mioyo ya watenda kazi utatambulika kwa wale wanaofanyiwa kazi. Roho zina kiu kwa ajili ya maji ya uzima. Msiwe vyombo vitupu. Kama utafunua upendo wa Kristo kwao, waweza kuwaongoza wenye njaa na walio na kiu kwa Yesu, naye atawapa mkate wa uzima na maji ya wokovu.Mar 105.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents