Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vijana ni Vitendea Kazi vya Mungu, Sura ya 113

    Ni vyema mwanadamu aichukue nira wakati wa ujana wake. Maombolezo 3:27.Mar 121.1

    Mungu anawaita vijana wakati wana nguvu zao za ujana kushirikiana naye katika kujikana nafsi, kujitoa mhanga na katika mateso. Kama wakiupokea wito huu, atawafanya kuwa vitendea kazi vyake kwa ajili ya kuokoa watu aliowafia. Lakini anataka wahesabu gharama na kuingia katika kazi wakiwa wanaelewa vizuri mazingira ambamo wanamtumikia Mkombozi aliyesulibiwa.Mar 121.2

    Kazi yetu ya kwanza ni kuifanya mioyo yetu ipatane na Mungu, na kisha tutakuwa tayari kutumika kwa ajili ya wengine. Katika siku za mwanzo kulikuwa na kujipeleleza sana miongoni mwa watendakazi wetu wenye bidii. Walishauriana pamoja katika maombi ya pamoja ya dhati na unyenyekevu ili wapate uongozi wa Mungu. . . Ujio wa Yesu umekaribia kuliko pale tulipoamini. Kila siku inayopita inatupunguzia siku moja zaidi ya kutangaza ujumbe na kuuonya ulimwengu. Sasa hivi inapasa kuwe na maombezi ya dhati mbele za Mungu, kuwe na unyenyekevu zaidi, usafi zaidi na imani kubwa zaidi.Mar 121.3

    Tuna kazi kubwa sana ya kufanya kwa ajili ya Bwana wetu, kulifungua neno la Mungu kwa wale walio katika giza na udanganyifu. Marafiki zangu vijana, fanyeni kana kwamba mna jukumu takatifu. Mnapaswa kuwa wanafunzi wa Biblia, mkiwa tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu. Kwa uungwana wenu wa kweli na wa Kikristo onesheni ushahidi kwamba mnajua ukweli wenye manufaa kwa watu watakaousikia. Kama ukweli huu mno ndani ya moyo, utajionesha usoni na katika mwenendo, katika kujitawala kwa utulivu na amani ambayo Wakristo tu wanaweza kuwa nayo. Wale walio na unyenyekevu wa kweli, na wale ambao akili zao zimepanuka kwa ukweli unaofunuliwa katika injili, watakuwa na ushawishi ambao utagusa watu. Watagusa akili na mioyo ya watu.Mar 121.4

    Sina shauku nyingine kubwa zaidi ya kuwaona vijana wetu wakijazwa na roho wa dini safi ambayo itawafanya wauchukue msalaba na kumfuata Yesu. Songeni mbele wanafunzi wa Kristo mlio vijana, mkiongozwa na msimamo sahihi, mkiwa mmevaa mavazi ya usafi na haki. Mwokozi wenu atawangoza hadi mahali ambapo talanta zenu zinafaa zaidi, pale ambapo mnaweza kutumika kwa ufanisi zaidi. Mnapoendelea na wajibu wenu, mnaweza kuwa na uhakika kwamba mtapokea neema ya kutosha kwa wakati wenu.Mar 121.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents