Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kazi kwa Ajili ya Rika Zote, Sura ya 114

  Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua Yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. 1 Yohana 2:14.Mar 122.1

  Kuna maeneo mengi ambamo vijana wanaweza kupata fursa kwa ajili ya juhudi zinazoweza kusaidia.... Katika kumailizia kazi hii ya injili, kuna eneo pana sana la kufanyia kazi; na sasa hivi kazi inahitaji watu wa kawaida kuliko wakati mwingine wo wote ule. Vijana pamoja na wale walio na umri mkubwa zaidi, wataitwa toka mashambani, toka katika mashamba ya mizabibu, na kutoka katika karakana, na kutumwa na Bwana kwenda kutoa ujumbe wake. Wengi kati yao wanaweza kuwa hawakupata fursa ya kuwa na elimu, lakini Kristo anaona sifa ndani yao ambazo zitawawezesha kutimiza kusudi lake. Kama wakiweka mioyo yao katika kazi na kuendelea kuwa wanafunzi, atawafanya wafae kumtumikia. . .Mar 122.2

  Hata kama talanta yako ni kubwa au ndogo sana, kumbuka ulicho nacho ndicho ulichopewa. Kwa njia hiyo Mungu anakupima, akikupatia fursa ya kuonesha uaminifu wako. Unawiwa naye kwa ajili ya uwezo wako wote. Uwezo wa mwili wako, akili zako na roho yako ni wake na uwezo huu unapaswa kutumika kwa ajili ya kazi yake. Muda wako, ushawishi wako, uwezo wako, ujuzi wako—vyote vinapaswa kutolewa hesabu kwake Yeye aliyetoa vyote.Mar 122.3

  Kijana anayefurahia kusoma neno la Mungu na kuomba hujazwa wakati wote na mikondo inayotoka katika Chemchemi ya uzima. Atafikia kimo cha juu kabisa cha uadilifu na upana wa fikra ambao wengine hawawezi kuwa nao. . . Wale wanaounganisha mioyo yao na Mungu kwa namna hiyo wanatambuliwa naye kama wana na binti zake. Wakati wote hufikia viwango vya juu zaidi, wakipata ufahamu wa juu zaidi juu ya Mungu na juu ya maisha ya milele, mpaka Mungu atakapowafanya wawe mifereji ya nuru na hekima kwa ulimwengu.Mar 122.4

  Tukiwa na jeshi la watenda kazi la namna hiyo, kama linaloweza kupatikana kwa vijana wetu, waliofundishwa kwa usahihi, ujumbe wa Mwokozi aliyesulibiwa na kufufuka, anayekuja hivi karibuni utapelekwa ulimwenguni kote kwa haraka sana. Mwisho utakuja upesi sana—mwisho wa mateso, huzuni na dhambi! Mar 122.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents