Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Msingi Hakika, Sura ya 119

    Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana anawajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu. 2 Timotheo 2:19.Mar 127.1

    Bwana atakuwa na watu waaminifu, wenye imani iliyo thabiti kama mwamba. Watakuwa mashahidi wake ulimwenguni, watakuwa vyombo vyake kwa ajili ya kazi maalum, yenye utukufu wakati wa maandalizi yake.Mar 127.2

    Wachungaji ambao wamekuwa wakihubiri ukweli kwa makini na kwa bidii wanaweza kukengeuka na kujiunga na majeshi ya adui. Lakini je, jambo hili linaufanya ukweli wa Mungu kuwa uongo? Mtume Paulo anasema, “La hasha, msingi wa Mungu ulio imara umesimama.” Imani na hisia za wanadamu vyaweza kubadilika; lakini ukweli wa Mungu hautabadilika kamwe. . .Mar 127.3

    Ni hakika kwamba tunao ukweli kama tulivyo na uhakika kwamba Mungu yu hai; na shetani, pamoja na hila na nguvu zake za kuzimu, hawezi kuubadilisha ukweli wa Mungu kuwa uongo. Ingawa yule adui mkuu atajaribu kwa uwezo wake wote kufanya neno la Mungu lisiwe na maana, ukweli unapaswa kuendelea kama taa inayowaka.Mar 127.4

    Mungu ametuchagua na kutuweka chini ya rehema zake. Je, tutadanganyika na maneno ya yule mwasi mkuu? Je, tutaamua kusimama upande wa Shetani na majeshi yake? Je, tutaungana na wavunjaji wa sheria ya Mungu? Badala yake ombi letu liwe: “Bwana, weka uadui kati yangu na yule joka.” Kama hatutakuwa na uadui na matendo yake ya giza, uzio wake wenye nguvu utatuzunguka, na mwiba wake uko tayari kila wakati kuchoma mioyo yetu. Tunapaswa kumchukulia kama adui anayeweza kuua. Tunapaswa kumpinga katika jina la Kristo. Kazi yetu bado inaendelea. . . Wale wanaoliitia jina la Kristo, wanapaswa kuvaa silaha za haki. . .Mar 127.5

    Wakati umefika ambapo tunapaswa kujua sisi wenyewe kwa nini tunamini vile tunavyoamini. . . Tunapaswa kujiwekea msingi mzuri kwa ajili ya wakati unaokuja, ili tuweze kuupata uzima wa milele. Tunapaswa kufanya kazi, siyo kwa nguvu zetu wenyewe, lakini kwa nguvu za Mwokozi wetu aliyefufuka. Je, tutafanya nini na tutathubutu kufanya nini kwa ajili ya Yesu?Mar 127.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents