Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu Atawaongoza Watu Wake, Sura ya 121

  Upitapo katika maji mengi mtakuwa pamoja nawe; na katika mito haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Isaya 43:2.Mar 129.1

  Mungu ana kanisa duniani, ambalo ni watu wake waliochaguliwa, wazishikao amri zake. Haongozi kundi liIilojitenga na kupotea, mmoja hapa na mwingine pale, lakini anaongoza jamii ya watu. Hakuna haja ya kuwa na mashaka, yaani kuhofia kwamba kazi haitafanikiwa. Mungu anaiongoza kazi yake, na atayaweka mambo yote sawa. Kama mambo yanahitaji kurekebishwa katika uongozi wa kazi, Mungu atashughulikia jambo hilo, na kusahihisha kila kosa. Tuwe na imani kwamba Mungu ataiongoza meli iliyobeba watu wa Mungu na kuifikisha salama bandarini.Mar 129.2

  Nilipokuwa nasafiri kutoka Portland, Maine kwenda Boston, miaka mingi iliyopita, tulikutwa na tufani, na mawimbi makubwa yakatusukasuka huku na kule. Mashada ya taa yalianguka na masanduku yakabingirika toka upande mmoja hadi mwingine kama mipira. Abiria walishikwa na hofu, na wengi walikuwa wakipiga kelele, wakingojea kifo.Mar 129.3

  Baada ya muda mwongoza meli aliingia. Nahodha alisimama karibu na mwongoza meli wakati mwongoza meli anashika usukani, akionesha hatari katika njia ambayo meli ilikuwa imeelekezwa. Yule mwongoza meli alisihi, “Shika usukani.” Nahodha hakuwa tayari kufanya hivyo, kwani alikuwa anajua kwamba alikuwa hana uzoefu. Hapo baadhi ya abiria wakaanza kufadhaika, na kusema kwamba walikuwa wanahofia kwamba yule mwongoza meli angetubamiza kwenye miamba. “Shika usukani.” Yule mwongoza meli alisihi tena; lakini nahodha na mwongoza meli walijua ya kuwa hawangeweza kuudhibiti usukani.Mar 129.4

  Unapoona kuwa kazi iko hatarini, omba, “Bwana, shika usukani. Tuvushe katika mashaka haya. Tufikishe salama bandarini.” Je, hatuna sababu ya kuamini kuwa Bwana atatufikisha kwa ushindi?. . .Mar 129.5

  Hamwezi kuelewa kwa akili zenu hafifu jinsi Mungu anavyofanya kazi. Mwacheni Mungu adhibiti kazi yake mwenyewe.Mar 129.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents