Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Kama Ilivyokuwa siku za Nuhu”, Sura ya 129

  Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Luka 17:26.Mar 137.1

  Nilioneshwa kuwa dunia ipo katika hali mbaya sana. Malaika wa rehema anakunja mbawa zake, akijiweka tayari kuondoka... Sheria ya Mungu inabatilishwa. Tunaona na kusikia juu ya machafuko na mfadhaiko, uhitaji na njaa, matetemeko na mafuriko; ukatili wa kutisha unatendwa na watu; badala ya hekima, misisimko inaongoza. Ghadhabu ya Mungu ipo juu ya wakazi wa dunia, ambao wanakuwa mafisadi kama walivyokuwa wakazi wa Sodoma na Gomora. Tayari moto na mafuriko vinaangamiza maisha ya maelfu na mali zao ambazo zilikusanywa kwa ubinafsi kwa kuwakandamiza maskini. Bwana ataikata kazi yake hivi karibuni na kuimaliza dhambi. Laiti taswira ambazo zimekuja mbele yangu zioneshazo uovu ambao umekuwa ukitendwa katika siku hizi za mwisho, zingeweka mguso wa ndani kabisa mawazoni mwa wale wanaodai kuwa watu wa Mungu.Mar 137.2

  Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. Bwana anaondoa vizuizi vyake duniani, na karibuni kutakuwa na mauti na maangamivu, kuongezeka kwa uhalifu, ukatili, matendo maovu dhidi ya matajiri ambao wamejitukuza wenyewe dhidi ya maskini. Wale wasio na ulinzi wa Mungu hawatapata usalama mahali popote. Mawakala wa kibinadamu Wanafundishwa na wanatumia uwezo wao wa ubunifu ili kuweka katika utendaji mpango ulio na nguvu sana ili kudhuru na kuua. . .Mar 137.3

  Ndugu zangu. . . , natoa wito kwenu. . . Maisha ya wengi ni dhaifu na yenye mwonekano mzuri kwa nje. . . Wanajifikiria wenyewe kama Wakristo, lakini hawajui kile kinachomaanishwa na maisha ya Kikristo. Je, kuwa Mkristo kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwa kama Kristo... Shirikiana na Mungu kwa kutenda kazi kwa kupatana naye. Fukuza kutoka kwenye hekalu la roho kila kitu ambacho kinaweka mwonekano wa sanamu. Huu ni wakati wa Mungu, na wakati wake ni wakati wako. Vipige vita vizuri vya imani, ukikataa kuwaza na kunena yatokanayo na kutokuamini. Ulimwengu unapaswa kusikia ujumbe wa onyo la mwisho.Mar 137.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents