Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Makutano walishangaa

  Watu walikuwa wakidhani kuwa furaha huja kwa kuwa na vitu vingi vya dunia hii. Furaha hiyo hufuatana na heshima na fahari pia. Kwa hiyo ilipendeza sana mtu kuitwa “Rabi”, na kuheshimiwa kama mtaalamu na mwalimu wa dini. Lakini Yesu alisema kuwa heshima ya ulimwengu ndiyo yote mtu awezayo kupata. Uwezo ulikuwa katika maneno yake. Wengi walikirishwa kwamba hakika Mwalimu huyu aliongozwa na Roho wa Mungu.TVV 164.2

  Baada ya kueleza jinsi furaha ya kweli inayopatikana, Yesu alieleza wajibu wa wanafunzi wake, kama mitume. Alijua kuwa watashambuliwa na ujumbe wao utakataliwa. Wanyenyekevu na wapole walioyapokea maneno yake walitazamiwa kusingiziwa, kuteswa, kufungwa, na kuuawa, lakini iliwapasa kuvumilia mpaka mwisho, na kuendelea mbele.TVV 164.3

  “Wa heri wateswao kwa ajili ya haki, kwa maana ufalme wa mbinuni ni wao”. “Mheri ninyi watu watakapowashutumu na kuwaudhi, na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinuni, maana ndiyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu”TVV 164.4

  Ulimwengu hupenda dhambi na kuchukia haki, na ndiyo iliyokuwa sababu ya fujo waliyomfanyia Yesu. Nuru ya Kristo ilimulika mahali pote na kuondoa giza lote lililofunika dhambi zao, na matengenezo ya hakika yalionekana jinsi yanavyotakiwa. Wale waliomhitaji Roho Mtakatifu vita ilianza mioyoni mwao; na wale waliong’ang’ania dhambi walianza kushindana na ukweli na walioufuata.TVV 164.5

  Hivyo wafuasi wa Kristo walishitakiwa kuwa ni wenye kuleta fujo kwa watu. Lakini ni kushirikiana na Mungu ndiko kulileta uadui kwa ulimwengu. Wao wanafuata njia ile iliyofuatwa na watu wema katika nchi. Kila aina ya jaribu wanalopata ni njia ya Mungu ya kuwatakasa. Kila shindano wanaloshindana huongeza furaha katika ushindi wao wa mwisho. Wakielewa mambo haya, majaribu yote wanayopata kwa ajili ya imani yao watayapokea kwa furaha, sio kwa malalamiko.TVV 164.6

  “Ninyi ni chumvi ya dunia” Hamwezi kuondoka katika nchi, ili kuepuka mateso. Hamna budi kuishi kati ya watu ili utamu wa upendo wa Mungu ndani yenu uweze kuwa kwao kama vile chumvi inavyohifadhi nchi isioze. Kama watumishi wa Mungu wangelihami-shwa kutoka nchini, dunia ingeachwa katika uharibifu. Waovu wanawiwa hapa duniani kwa mibaraka ya watu wa Mungu, ambao wanawadharau na kuwatesa. Lakini Wakristo wakiwa ni kwa jina tu, wala si kwa hakika, hufanana na chumvi iliyoharibika. Kwa kutomwakilisha Mungu vilivyo, huwa wabaya kuliko wasioamini.TVV 165.1

  “Ninyi ni nuru ya ulimwengu” Wokovu ni kama mwanga wa jua, unaenea katika ulimwengu wote.TVV 165.2

  Dini ya Biblia siyo ya kufunikwa ndani ya kitabu, au kufungiwa katika jengo la kanisa. Dini ni ya kutakasa maisha ya kila siku, na kujidhihirisha katika hali zote za kushirikiana na watu. Kanuni za haki lazima zihifadhiwe mioyoni mwa watu wote. Maisha ya unyofu, hali kamilifu na moyo mkarimu, ndiyo yanayoangazia ulimwengu, kama nuru ya ulimwengu.TVV 165.3

  Yesu alijua kuwa wapelelezi wako tayari kuchukua kila neno lake ambalo litawafaa kutimilizia kusudi lao. Hakusema jambo lolote kuhusu maagizo ya Mungu, ambalo linahusu imani. Kristo mwenyewe ameeleza mambo yahusuyo sheria ya Mungu, na sheria yakawaida. Hakuja kuharibu mafundisho yake mwenyewe. Wakati alipokataa mambo muhimu yaliyotolewa kwa Waebrania.TVV 165.4

  Maneno ya Mwokozu yalikuwa kama ni ya uzushi kwa Mafarisayo. Alipofagilia mbali takataka zilizochanganyikana na na ukweli, walidhani kuwa alikuwa akifagia ukweli wenyewe. Alisoma mawazo yao, na kuwajibu kwamba “Msidhani kuwa nalikuja kuondoa sheria, au manabii. Sikuja kutangua, bali kutimiza” Kazi yake ilikuwa kuonyesha utakatifu wa sheria ambayo wao walisema kuwa ameivunja. Kama sheria ya Mungu imevunjwa au imetanguliwa, basi Kristo asingeliteseka kwa ajili ya maasi yetu. Alikuja kueleza uhusiano wa sheria na binadamu, na kuifikiliza katika maisha yake ya kuitii.TVV 165.5

  Utii huleta furaha.TVV 166.1

  Mungu huwapenda wanadamu. Ili kusudi kutukingia tusikumbwe na matokeo ya uasi, amedhihirisha kanuni ya haki. Sheria inapopokewa katika Kristo, hutuinua juu ya uwezo wa tamaa ya asili na maelekeo yake, na hutuinua juu ya majaribu yaletayo dhambi. Mungu alitupa amri zake, ili tunapozitii tupate furaha.TVV 166.2

  Katika mlima wa Sinai Mungu alijijulisha mwenyewe jinsi utakatifu wake na tabia yake vilivyo, ili kwa kuona tofauti ilivyo wapate kuona jinsi walivyo wenye dhambi sheria ilitolewa ili kuwathibitishia dhambi, na kufunua haja yao ya kuhitaji Mwokozi. Kazi hii ingali ikifanyika vile vile. Roho Mtakatifu anapowafunulia wanadamu hitaji lao la damu ya Kristo yenye kutakasa na kuwahesabia haki, sheria bado ndiyo inatuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. “Sheria ya Bwana ni kamilifu huiburudisha nafsi.” Zaburi 19:7.TVV 166.3

  “Mpaka mbingu na nchi zitakapopita, yodi moja au nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Jua liwakalo, na nchi isimamayo imara ni mashahidi wa Mungu kwamba sheria yake ni ya milele. Hata kama mbingu na nchi zitapita, lakini sheria ya Mungu itadumu. Kawaida ya mfano, kwamba Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu, itapita wakati wa kifo cha Yesu, lakini amri za Mungu zitadumu kama kiti chake cha enzi kidumuvyo.TVV 166.4

  Maisha ya Mwokozi ya utii yalithibitisha kwamba sheria inaweza kushikwa na wanadamu, na ilionyesha uzuri wa tabia itakayokuzwa. Kwa upande mwingine, wale wanaovunja amri za Mungu, humsaidia Shetani anayedai kuwa sheria ya Mungu haiwezekani kushikwa. Kama wakikaribishwa huko mbinguni, wataleta manung uniko na uasi, na kuharibu uzuri wa ulimwengu. Hakuna mtu yeyote atakayevunja kanuni yoyote ya sheria atakayeingia katika ufalme wa mbinguni.TVV 166.5

  Siku zile Kristo alipokuwapo ulimwenguni udanganyifu mkuu wa watu ulikuwa kwamba, ukikubali tu dini kwa juu juu, utapata haki. Katika maisha yote ya kibinadamu kukubali dini ya juu juu tu na kukariri kanuni za kweli hakukuleta wokovu kwa mtu yeyote, wa kuzaa matunda ya pasayo toba.TVV 166.6

  Matokeo ya kujua tu maneno ya dini peke yake huleta chuki kwa wale walio na imani ya kweli. Sura yenye giza zaidi katika historia ni ile inayohusu maasi makuu yaliyotokana na wenye dini. Mafarisayo walidhani kuwa wao ndio wakuu wa dini kuliko wengine wote ulimwenguni, lakini kujidai kwao kuliwaongoza mpaka wakamsulubisha Bwana wa utukufu. Watu wengi hujidai kuwa ni wenye dini, lakini dini yao hiyo isipowafanya kuwa waaminifu hasa, wenye utu wema, wavumilivu, wastahimili, wenye mawazo ya kimungu, huwa laana kwao tu, na kwa mivuto yao huwa balaa kwa ulimwengu.TVV 166.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents