Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Imani hai huponya

    Kuzungumzia dini kwa njia ya bahati nasibu tu, kuomba vivi hivi bila kusikia haja rohoni, ni kazi bure. Imani ya juu juu ambayo ni ya jina tu, inayomtaja kristo kuwa ni Mwokozi wa ulimwengu basi, haiwezi kuleta uhai wa roho ya mtu. Imani siyo elimu ya kujua kawaida za dini tu, wala haitoshi kusema kuwa namwamini Yesu Kristo. Yatupasa tumwamini na kumtegemea. Imani ya kweli ni hali ya kazi ya maagano ya lweli ya muungano kati ya Mungu na mtu. Kuwa na uhusiano halisi kati ya Mungu na sisi. Imani ya kweli ni kutumaini kwa kweli, kunakofanya ushindi katika maisha ya mtu.TVV 191.1

    Baada ya kumponya mwanamke yule, Yesu alitaka akiri mibaraka aliyopokea. Kipaji kinachotolewa na injili si cha siri. Ungamo letu la uaminifu wake ni chombo cha mbinguni cha kumdhihirisha Kristo ulimwenguni. Mambo muhimu katika dini yetu ni ule uaminifu wetu wa kweli katika kanuni za Mungu. Isaya 43:12. Ukubali wa neema yake unapoungwa na hali yetu ya kikristo katika maisha yetu, huwa uwezo unaoleta wokovu kwa watu.TVV 191.2

    Watu wenye ukoma kumi walipomjia Yesu wakitaka kuponywa, waliponywa. Lakini ni mtu mmoja tu aliyerudi kushukuru. Ni watu wangapi leo hufanya mambo kama hayo? Bwana humponya mgonjwa, huwatoa watu katika hatari, huwaagiza malaika zake wawaepushe watu na hali za lika namna, na kuwalinda na uharibifu wa maradhi, (Zaburi 91:6); ni hivyo hawajali upendo huo ulio mkuu. Kwa kutokuwa na shukrani hufunga mioyo yao isiione neema ya Mungu. Ni kwa ajili ya faida yetu tu, kulinda vipawa vya Mungu anavyotupatia. Hivyo imani ni nguvu inayoimarishwa. Basi tukumbuke upendo wa Mungu na fadhili zake kwetu. Tunapojikumbusha fadhili za Mungu, na jinsi anavyotntendea, husema: “Nimrudishie Bwana nini, kwa ukarimu wake wote alionitendea?” Zaburi 116:1.TVV 191.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents