Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Lazima tukabiliane na upinzani

  Yesu akiendelea na mafundisho kwa wanafunzi wake, alisema: “Jihadharini na wanadamu.” Wasingaliwategemea watu ambao hawamjui Mungu, na kutafuta mashauri kwao, maana kufanya hivi kungewapa watumishi wa Shetani nafasi ya kuwaingilia. Mavumbuzi ya wanadamu kila mara huwa kunyume cha kazi ya Mungu, na mipango yake. Watumishi wa Mungu wanapotegemea mashahauri ya watu na mipango yao, humdharau Mungu kabisa, na kuisaliti kazi ya Injili, wasipomtegemea roho Mtakatifu awaongoze.TVV 194.2

  “Watawapeleka mabarazani, . . . nao watawakokota mbele ya maliwali na mbele ya wafalme, kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda wangu, na mbele ya watu wa mataifa. Watumishi wa Kristo wataletwa mbele ya wakuu wa dunia hii, ambao pasipo mambo haya wasingalisikia neno la Mungu. Wanaposikia mambo ya uongo kuhusu kazi ya watumishi wa Mungu, na imani ya wanafunzi wa Kristo, njia ya pekee ya kujua uhakika wa mambo, ni kuwatia majaribuni wafuasi wa Mungu kwa ajili ya imani yao. Yesu alisema. “Mtapewa katika saa hiyo mambo mtakayosema. Maana si ninyi msemao, bali roho wa Baba yenu ndiye asemaye ndani yenu.” Wale wanaoikataa kweli ya Mungu watainuka na kuwashitaki wanafunzi wa Yesu. Lakini watu wa Mungu wanapasea kuwa na roho ya upole kama Bwana wao alivyokuwa. Hivyo watawala wataona tofauti baina ya watumishi wa Shetani, na wajumbe wa kristo.TVV 194.3

  Wafuasi wa Kristo wasingetayarisha usemi wao watakaosema, wanapofikishwa katika majaribu. Robo Mtakatifu atawaongoza jinsi ya kusema ukweli utakiwao. maarifa yaliyopatikana kwa kujifunza ukweli halisi katika maandili matakatifu, utawaka na kukumbukwa katika mawazo yao. Lakini kama mtu yeyote ambaye hakujali kujishughulisha na maneno ya Kristo, asidhani kuwa Roho Mtakatifu atamletea kumbukumbu yoyote katika mawazo yake.TVV 194.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents