Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tutafanyaje majaribu yatujiapo

  Wanafunzi wa Kristo wangesalitiwa hata na watu wajamaa zao. “Mtachukiwa na watu waote kwa ajii ya jina langu; lakini atakayestahimili mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka.” Lakini aliwaagiza kwamba wasijiweke wenyewe katika mateso bila sababu. Yeye mwenyewe kila mara aliacha kazi katika sehemu moja ili ifanywe na wengine, kwa kuepuka watu wanaotaka kumwangamiza. Vivyo hivyo watumishi wake, wasingevunjwa moyo na mateso, ila wangetafuta mahali pengine pa usalama ili waendelee kufanya kazi ya injili.TVV 195.1

  Lakini katika mateso yoyote, watumishi wa Kristo, lazima wadharau hali ya kujificha na kuepa mateso iwapo ni lazima. Hawawezi kuiacha kweli ili kuepa mateso. Yesu aliseema, “Niwaambiayo katika giza, yatangazeni katika nuru, na yale mnayosikia kwa siri ninyi yatangazeni juu ya nyumba.”TVV 195.2

  Yesu kamwe hakutaka usalama kwa njia ya kukubaliana na mambo yasiyokuwa ya kweli. Roho yake iliwahurumia wanadamu wote na kuwafadhili, lakini hakukubaliana na matendo yao ya dhambi, alinyamaza tu wakati walipoendesha mambo yatakayowaharibu. aliwafundisha ili wawe watu wa kweli, wanaochuchumilia faida ya juu. Watumishi wa Kristo wametiwa kazi ya jinsi hiyo. Hivyo lazima wajihadhari sana wasije wakashusha kanuni za kweli wakati wanapojaribu kuleta amani. Amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutelemsha kanuni za unyofu. “Msiwaogope wenye kuua mwili, wasiweze kuua roho.” Hofu yao ingekuwa kuisaliti kweli ambayo kwayo, Mungu hutukuzwa, kwa njia yao.TVV 195.3

  Shetani hujitahidi kuwatilia watu mashaka. Huwashawishi watende dhambi, halafu waonekane kuwa ni wachafu mno. hawawezi kuonekana mbele ya Mungu mtakatifu, ambaye ni Baba wa mbinguni, bwana anafahamu haya yote. Yesu aliwathibitishia wanafunzi wake huruma za Mungu, kwamba hakuna kitu hata kidogo kisichojaliwa mbele zake.TVV 195.4

  Biblia hutuonyesha kwamba Mungu yuko juu, mahali patakatifu (Isaya 57:15) wala hakai tu bila shughuli, akinyamaza kimya ila anazungukwa na viumbe maelfu vyenye maarifa, ambao ni watakatifu, wanaofanya mapenzi yake. Sisi hatuwezi kuelewa na maajabu yake. Huunganika na sehemu zote za utawala wake na kuwasiliana nao, pamoja na dunia yetu pia. Mungu huinama na kusikiliza malalamiko ya mwenye dhiki, ingawa anakaa kwenye kiti chake cha enzi. Hujibu kila ombi la mtu mwenye haja, na kusema: “Mimi hapa.” Huwainua watu waliodidimia na wenye dhiki. Malaika kutoka mbele yake huenda kumwokoa kila mtu aliye katika majaribu na mateso.TVV 195.5

  Yesu alisema: “Jinsi mnavyonikiri mbele ya watu, ndivyo nami nitakavyowakiri mbele za Baba yangu na mbele ya malaika zake.” Mtakuwa mashahidi wangu duniani, nami nitawawakilisha mbinguni. Baba haangalii tabia zenu chafu, ila huwaangalia mmevikwa haki yangu ambayo ni ukamilifu wa tabia yangu. Na kila mtu anayeshiriki dhabihu ya kujitolea kwangu, atakuwa mshiriki wa utukufu na furaha ya ukombozi.TVV 196.1

  Mtu ambaye atamwungama Kristo, lazima Kristo awe anaishi ndani yake. Mitume wake lazima wawe wakinena kwa ufasaha mafundisho yake. Lakini wasipokuwa nayo tabia ya kikristo halisi, tabia ya unyenyekevu na upendo, hawawezi kumwungamia. Roho ambayo ni kinyume cha roho yake humkana. Watu humkana Kristo kwa kusema misemo mibaya, kwa maongezi ya kijinga, kwa maneno ya ovyo ambayo siyo ya kweli, au kwa maneno yasiyo mema. Wanaweza kumkana kwa kutosaidia mzigo wa maisha ya watu, na kwa kujiunganisha na kawaida za dunia, na kwa hali isiyokuwa ya utu mwema, na kwa njia ya kukuza hali ya ubinafsi, na kwa kuwa na mashaka, na kuwa na uchokozi. “Mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.”TVV 196.2

  Mwokozi alisema: “Sikuja kuleta amani duniani, ila kuleta upanga.” mashindano siyo mambo yafaayo kwa injili, bali ni kinyume cha injili. Katika mateso yote, yaliyo magumu ni ya nyumbani. Mfarakano wa watu wa nyumbani na marafiki. Lakini Yesu alisema: “Apendaye baba au binti kuliko mimi hanifai. Na mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata hanifai.”TVV 196.3

  “Awapokeaye ninyi, hunipokea mimi, na yeye anipokeaye mimi humpokea aliyenituma.” Hakuna tendo la wema litendwalo kwa jina lake, lisilopewa thawabu. Huongeza wana walio wadhaifu wa jamaa ya Mungu. Atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi, amini nawambieni, hatakosa kupata thawabu yake.”TVV 196.4

  Hivyo ndivyo Mwokozi alimaliza mafundisho yake. Wanafunzi kumi na wawili waliochaguliwa wakaenda nje, kama alivyokwenda kuhubiri injili kwa miaskini ... na kuwaponya waliovunjika mioyo, kuhubiri uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya vipofu kuona. Luka 4:18.TVV 197.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents