Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Pumziko liliwaburudisha

  Wakati ambao Yesu na wanafunzi wake walitumia katika mapumziko haukuwa wakati wa anasa. Waliongea pamoja kuhusu kazi ya Mungu na mambo yatakiwayo kufaulisha. Kristo aliwasahihisha makasoro yao, na kuwaonyesha jinsi ifaayo ya kukutana na watu. Walitiwa nguvu na uwezo wa Uungu na wakawa na ushujaa na moyo mkuu.TVV 199.4

  Yesu aliposema kwamba, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache”, hakuwa na maana ya kufanya kazi wakati wote bila kukoma, bali “Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watendakazi katika mavuno yake.” Mathayo 9:38. Mungu hapendi watu wachache tu wabebe mzigo mzito wa kuwalemea katika kazi yake, wakati huo huo wengine hawataabiki kwa lolote, kuhusu roho za watu.TVV 199.5

  Maneno ya Kristo ya huruma, yanawahusu watenda kazi wake leo pia. “Njooni peke yenu hapa . . . mpumzike kidogo.” Sio hekima kufanya kazi ya kuwahudumia watu kwa mambo ya kiroho bila kupumzika, maana kwa jinsi hii utawa wa mtu huachwa bila kushughulikiwa, na nguvu za mwili huchoshwa sana. Kujitoa nafsi kunahitajika, lakini hadhari lazima iwepo, ama sivyo Shetani atapata nafasi ya kupenya na kumdhoofisha mtu, na kazi ya Mungu itakuwa na madoa.TVV 199.6

  Shughuli zinapozidi za kazi ya Mungu, na watu wakifanikiwa katika kazi ya Mungu, kuna hatari ya kuwa na maombi machache na imani chache pia. Mambo hayo huelekea kuwa hivyo. Huelekea kuwa na kumtegemea Mungu kidogo, na kutegemea shughuli hizo. Uwezo wa Kristo ndio unaowezesha kazi kufanyika. Inatupasa tupate wakati wa kutafakari, kuomba, na kujifunza neno la Mungu. Kazi inbayotimilika kwa njia ya maombi mengi, na kwa uthibitisho wa Ksristo, ndiyo itakayofaulu mpaka mwisho kupata sifa bora.TVV 200.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents