Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi kiburi cha Simon kilivyoshushwa

  Simoni aliguswa na wema wa Yesu ambao uliomfanya asikemee wazi mbele ya wageni wake. Hakutendewa jinsi alivyotaka Mariamu atendewe. Aliona kuwa Yesu alitafuta kwa wema na huruma kuutiisha moyo wake. Kukemewa kwa ukali, kungalishupaza toba, lakini onyo la upole kulimsadikisha dhidi ya kosa lake. Aliona ukubwa wa deni analowiwa na Bwana wake. Farisayo huyu jeuri alitubu, akawa mnyenyekevu, na mwanafunzi aliyejikana nafsi. Kristo alijua hali iliyoongoza maisha ya Mariamu. Angaliweza kuzima kila cheche ya tumaini rohoni mwake, lakini hakufanya hivyo. Alikuwa amemnyanyua kutoka katika kukata tamaa na maangamizi. Mara saba alikuwa amesikia Yesu akikemea mashetani yaliyokuwa yakimtawala moyoni na akilini. Alikuwa amemsikia akimlilia Baba yake kwa nguvu zote kwa niaba yake. Mariamu alijua jinsi dhambi ilivyo kinyaa kwa weupe wa usafi wake Yesu, na kwa uwezo wa Yesu alikuwa ameshinda hali hiyo.TVV 317.3

  Wakati ilionekana kwa hali ya kibinadamu kuwa hali ya Mariamu ni isiyo na tumaini, lakini Kristo aliona ndani ya Mariamu uwezekano wa hali bora. Mpango wa ukombozi umempa mwanadamu uwezekano mkubwa, na katika maisha ya Mariamu mambo haya yangewezekana. Kwa njia ya neema yake Yesu, Mariamu akawa mshirika wa asili ya Uungu. Aliyekuwa ameanguka, ambaye moyo wake umekuwa makao ya mashetani, alifikishwa karibu na Mwokozi katika ushirika na utume. Mariamu aliketi miguuni pake, na akajifunza kwake’ alimpaka mafuta, na kumnawisha miguu yake kwa machozi yake; Mariamu alisimama kando ya msalaba, na akanifuata mpaka ka-burini; Alikuwa wa kwanza kufika kaburini na kumtangaza Mwokozi aliyefufuka.TVV 318.1

  Yesu hujua hali zote za kila mtu. Unaweza kusema kuwa u mwenye dhambi sana, sana. Labda ndivyo; lakini jinsi ulivyo ovyo, ndivyo unavyonihitaji zaidi Yesu yeye hamzuii mwenye machozi na toba Yeye huwasamehe wale wote wanaomjia kupata msamaha na kufanywa upya.TVV 318.2

  Watu wanaomwendea, kama kimbilio, Kristo huwaunganisha katika asili ya Uungu wake. Hakuna mtu au malaika mwovu atakayewashutumu. Watasimama ubavuni mwake Mwondoa dhambi mkuu, katika nuru iangazayo kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu.TVV 318.3

  “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; na zaidi ya hayo amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.” Warumi 8:33, 34.TVV 318.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents