Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    63 — Yesu Atangazwa Kuwa Mfalme wa Israeli

    Miaka mia tano kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, nabii Zekaria alitabiri kuja kwake kama mfalme wa Israeli. Alisema: “Furahi sana, Ee binti Sayuni, Piga kelele, Ee binti Yerusalemu, tazama mfalme wako anakuja kwako; ni mwenye haki naye ana wokovu, Ni mnyenyekevu, amepanda punda Naam, mwana punda mtoto wa punda.” Zekaria 9:9. Yeye aliyeukataa ufalme na heshima yake, sasa aliingia Yerusalemu kama mrithi aliyetabiriwa wa kiti cha ufalme wa Daudi.TVV 319.1

    Katika siku ya kwanza ya juma, Kristo aliingia kwa shangwe mjini: Watu wengi waliokuja Bethania ili kumwona walifuatana naye. Wengine waliokuwa wakienda katika Pasaka waliungana naye pia. Shangwe ilionekana mahali pote hata miti ilitoa maua, na mwamko wa kutawazwa kwa mfalme mpya ulionekana kwa watu.TVV 319.2

    Yesu alikuwa amewatuma wanafunzi wawili waende wakamletee punda na mwana punda. Ingawa ng’ombe walioko milimani elfu, elfu ni mali yake, (Zaburi 50:10) alimtegemea mgeni ili amfadhili, na mnyama wa kupanda ili aingie Yerusalemu kwa shangwe, kama Mfalme. Walakini hata hivyo Uungu wake ulidhihirishwa katika wakati uliotajwa. Kama alivyotabiri “Bwana ana haja nao,” alipewa mara moja. Wanafunzi walitandika nguo zao juu ya punda, wakampandisha Bwana wao juu yake. Kila mara Yesu alikuwa akitembea kwa miguu, na sasa wanafunzi walishangaa kutaka kumpanda punda. Lakini hamu yao iliwaka kuwa ataingia mjini ajitangaze kuwa mfalme mwenye uwezo. Mashangilio ilijaa mji wote, na matazamio ya watu yaliamshwa kwa kiwango cha juu.TVV 319.3

    Kristo alifuata desturi ya Kiyahudi ya kuingia kwa heshima mjini, kama mfalme. Unabii ulitabiri kwamba Masihi ataingia hivyo kwa shangwe kama mfalme. Mara moja alipopanda punda watu wakamtukuza kama Masihi Mfalme wao. Wanafunzi na makutano waliona katika dhana zao majeshi ya Warumi yakifukuzwa kutoka katika nchi yao, na Waisraeli wanakuwa taifa huru tena. Wote walishindana katika kumtukuza kwa heshima kuu. Badala ya kumpa zawadi za gharama, walitandika mavazi yao chini kama zulia njiani na kutawanya matawi ya mizeituni na mitende. Wakiwa hawana bendera ya kifalme kupeperusha, walikata matawi mapana ya mitende, kama nembo ya Asili ya ushindi, na kuyapeperusha juu.TVV 319.4

    Watazamaji waliochanganyikana na kundi, waliuliza: “Huyu ni nani? Hoi lioi hii yote ni ya nini? Walijua kuwa Yesu amekataa juhudi zote za kumtawaza kuwa mfalme, na walishangaa kugundua kuwa huyu ndiye. Ni kitu gani kilichombadilisha yeye aliyekuwa ametangaza kuwa ufalme wake siyo wa dunia hii?TVV 320.1

    Kutoka kwa makutano waliokuja kuhudhuria Pasaka, maelfu walimsalimu kwa kumpungia matawi ya mitende na kumwimbia nyimbo takatifu. Makuhani Hekaluni walipiga tarumbeta ya kuwaita watu kwenda katika ibada, ya jioni, lakini ni watu wachache tu ndio walioitikia kwenda. Wakuu wakasemezana: kwa hofu “Ulimwengu umekwenda nyuma yake.”TVV 320.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents