Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi ya kujengeka baada ya kuvunjika

  Kwa wale wanaomwamini, Kristo ni msingi ulio imara. Wameanguka mwambani na “wamevunjika”. Kuanguka mwambani na kuvunjika, maana yake ni kuacha hali ya kujiona kuwa mwenye haki, ni kumwendea Kristo kwa unyenyekevu, kama mtoto na kutubu makosa yetu yote, na kuamini upendo wake wa msamaha. Kwa imani na utii hujenga juu ya Kristo, ambaye ni msingi imara.TVV 335.2

  Juu ya msingi huu ambao jiwe hai kuu la pembeni ni Yesu watu wote hujenga kwake, yaani Wayahudi na watu wa mataifa pia. Unawatosha wote, na kuchukua uzito wa ulimwengu wote. Wote wanaojiunga naye na kujenga juu ya msingi huu huwa mawe yaliyo hai. (Soma 1 Petro 2:5).TVV 335.3

  Kwa wale wanaojikwaa kwa neno, huasi. Kristo ni mwamba wa kujikwaa. Kama jiwe lililokataliwa, alichukua aibu zote. “Alidharauliwa na kukataliwa na watu, wala hakuhesabiwa kuwa ni kitu.” (Soma Isaya 53:3.) Lakini kwa kulufuka kutoka kwa wafu alihesabiwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu. (Tazama Warumi 1:4.) Atakaporudi ataonekana kuwa Bwana wa mbingu na nchi, jiwe lililokataliwa na waashi, sasa ni jiwe kuu la pembeni, mfalme wa ulimwengu.TVV 335.4

  Mtu ambaye ataangukiwa na jiwe hili atasangwasagwa. Waliomkataa Kristo, walishuhudia maangamizo ya mji wao na nchi yao. Utukufu wao ukatawanyika kama mavumbi. Mwamba ambao wangalijengea ungekuwa usalama wao. Zilikuwa ni rehema za Mungu zilizodharauliwa na wema uliodhihakiwa. Watu walijiweka wenyewe kuwa kinyume na Mungu, na yote yale yaliyokuwa yawe wokovu wao yakawa maangamizi yao.TVV 336.1

  Kusulubishwa kwa Kristo na Wayahudi kulichanganyikana na kuangamizwa Yerusalemu. Damu ya Yesu waliyomwaga ndiyo iliyokuwa uzito uliowazamisha kwa maangamizi.TVV 336.2

  Hivyo katika siku ya mwisho wakati hukumu ya Mungu itakapowakalia walioikataa neema ya Mungu, Kristo ataonekana kama mlima wakulipiza kisasi. Utukufu wake, ambao kwa watakatifu ni uzima, kwa waovu utakuwa ni moto wa kuteketeza. Kwa ajili ya upendo uliokataliwa, neema iliyodharauliwa, wenye dhambi wataangamizwa. Hekalu lililochafuliwa, mwana mkaidi, wakulima waovu, wajenzi wakorofi, wote hupata mfano katika njia ya kila mwenye dhambi. Asipotubu hukumu iliyowakabili itakuwa yake.TVV 336.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents