Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sauti ya Mungu Ilisikika

  Ndipo ukaja utukufu wa uungu katika mapenzi ya Babaye, Akasema, “Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako.” Ni kwa kifo cha Kristo tu, ndio utawala wa Shetani ungeangushwa, mwanadamu akombolewe na Mungu atukuzwe. Yesu aliikubali dhabihu, akakubali kuteseka kama Mchukua Dhambi. Sauti ikatoka ndani ya wingu liliotanda juu ya kichwa chake; “Nimelitukuza nami nitalitukuza tena.” Katika mateso ya kiungu kibinadamu yajayo Kristo, atalitukuza jina la Baba yake. Sauti iliposikika nuru ilimzunguka Kristo, kana kwamba mkono wa nguvu za Uungu uliomzungushia ukuta wa moto. Hakuna mtu aliyethubutu kusema kitu. Wote walisimama wakimwangalia Yesu. Ushuhuda wa Baba ukiwa umetolewa, wingu liliinuka na kutawanyika hewani.TVV 351.4

  Wayunani waliokuwa wamekuja kumwulizia waliliona wimgu, wakaelewa maana yake na kumtambuaTVV 352.1

  Kristo, hakika; kwao alidhihirishwa kama Aliyetumwa na Mungu. Sauti ya Mungu ilikuwa imesikika wakati wa Ubatizo wa Yesu, na wakati Yesu alipogeuka sura mlimani. Sasa kwa mara ya tatu ilisikika katika kundi la watu wengi. Yesu alikuwa ametoa wito wake mara ya mwisho, na kutamka maafa yatakayowapata Wayahudi. Na sasa Mungu anamtambua yule aliyekataliwa na Israeli. Yesu akasema: “Sauti hiyo haikuwako kwa ajili, yangu, bali kwa ajili yenu. ” Ilikuwa ni ushuhuda kutoka kwa Mungu kwamba Yesu alikuwa amesema ukweli, na kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.TVV 352.2

  “Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa,” Kristo aliendelea kusema, “mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje,” “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa”. Ikiwa mtakuwa kipatanisho kwa dhambi za wanadamu, ulimwengu utaangazwa. Uwezo wa Shetani kuwashikilia watu utavunjika. Sura ya Mungu iliyoharibiwa itarudishwa kwa wanadamu, na jamii ya wenye haki waaminio watayarithi makao ya mbinguni. Mwokozi aliuona msalaba, jinsi ulivyo wa ukatili na aibu yake pamoja taabu zake, ukiwaka kwa utukufu. Lakini ukombozi wa mwanadamu si yote yaliyomalizwa na msalaba. Upendo wa Mungu unadhihirishwa ulimwenguni. Doa lililotiwa mbinguni na Shetani linaondolewa kwa milele. Malaika na watu watavutwa kwa Kristo. “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,” Alisema “nitawavuta wote kwangu.”TVV 352.3

  Watu wengi walikuwa wamemzunguka Kristo alipokuwa akisema maneno haya; “Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini.”TVV 352.4

  Ishara zisizohesabika zilikuwa zimetolewa lakini watu walifumba macho yao na kufanya mioyo migumu. Kwa vile sasa Baba mwenyewe alikuwa amenena na hawakuwa na la zaidi kuuliza, bado walikataa kuamini.TVV 352.5

  “Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi”. Katika kujikinga na fedheha na aibu walimkana Kristo na kukataa toleo la uzima wa milele. Ole kwa wale, ambao hawakutambua wakati wao uliowajilia! Taratibu na kwa huzuni Kristo aliondoka hekaluni milele.TVV 352.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents