Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Dhambi ya Siri ya Petro

    Sasa sauti ya Petro ilisikika ikipinga “Hata wajapo kunguwazwa wote, lakini siyo mimi” Yesu alikuwa amemwonya kwamba usiku ule atamkana Mwokozi wake. Sasa akarudia onyo lake akisema, “Amini, nakuambia wewe, Leo usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili utanikana mara tatu.” Lakini Petro “akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe, hata hivyo sitakukana kamwe. Na wote wakasema vile vile.” Marko 14:29-31).TVV 381.5

    Petro aliposema kuwa atamfuata Bwana wake hata kama ni gerezani au kifoni, alisema kweli, lakini hakujifahamu alivyo. Katika moyo wake kulifichika chembechembe za uovu ambazo hali halisi ya mambo ingezifunua wazi. Asipotahadharishwa juu ya hali hiyo ingemwingiza katika hatari ya kupotea. Mwokozi aliona ndani yake kujipenda ambako kungelemea upendo wake kwa Kristo. Petro alihitaji kuwa na hali ya kutokujiamini na kuwa na imani kamili katika Kristo. Wakati akiwa katika bahari ya Galilaya, alipotaka kuzama, alilalama na kusema: “Bwana uniokoe.” Hivyo hivyo na sasa kama angalilia na kusema niokoe katika hali hii ya kujitumainia, angalilindwa. Lakini Petro akaona kama ukatili kule kutoaminika na hivyo akazidi katika kujiamini kwake.TVV 382.1

    Yesu hakuweza kuwaokoa wanafunzi wake katika majaribu, lakini pia hakuwaacha bila faraja. Kabla ya kumkana walikuwa na uhakika wa msamaha. Baada ya kifo na ufufuo wake Kristo walielewa kuwa wamesamehewa na walikuwa wapenzi wa moyoni wa Kristo.TVV 382.2

    Yesu na wanafunzi wake walikuwa njiani kwenda Gethsemane, chini ya Mlima wa Mizeituni. Mwezi ulikuwa uking’aa na bustani ya mizeituni iliyositawi ilionekana kwake vizuri sana. Yesu akiwaelekeza wanafunzi wake kwa mizabibu hiyo, alisema “Mimi ndimi mzabibu wa kweli.” Mzabibu uliozungukwa kwa vikonyo unamwakilisha yeye Mwenyewe. Miti ya minazi, mierezi na mpingo husimama peke yake; haihitaji kitu cha kuitegemeza. Lakini mizabibu hujisokotesha katika fito na hivyo kupanda kuelekea mbinguni. Vivyo hivyo na Kristo katika hali yake ya kibinadamu aliegemea uwezo wa Mungu. “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.” Yohana 5:30.TVV 382.3

    “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.” Katika vilima vya Palestine Baba yetu wa mbinguni alikuwa ameupanda Mzabibu huu mzuri. Watu wengi walikuwa wakivutiwa na uzuri wa Mzabibu huu na kuusifia kuwa ni wa kutoka mbinguni. Lakini wakuu wa Israeli waliukanyaga mmea huu chini ya miguu yao miovu. Baada ya watu kudhani kwamba wameuua, Mkulima wa mbinguni aliuchukua na kupanda tena upande mwingine wa kitalu. Shina la Mzabibu lisingeonekana tena. Lilifichika lisionekane na watu wakorofi. Bali matawi yake yalining’inia ukutani ili kupitia kwayo chipukizi ya mizabibu mingine ipandikizwe kwa ule Mzabibu tena. Yesu alisema kuwa mwungano wa shina la mzabibu na matawi hufananishwa na uhusiano ambao wafuasi wake wanapaswa kudumisha kwake. Mche hupandikizwa katika Mzabibu ulio hai na hivyo kitembwe kwa kitembwe chelewa kwa chelewa hukua na kuzama katika shina la Mzabibu.TVV 382.4

    Ndivyo moyo hupata uhai kwa kuungana kwake na Kristo. Mwenye dhambi huunganisha udhaifu wake pamoja na nguvu za Kristo, uwazi wake kwa ujazo wa Kristo. Ndipo hupata nia ya Kristo. Ubinadamu wa Kristo umegusa wetu na ubinadamu wetu umegusa Uungu.TVV 383.1

    Mwungano huu lazima udumishwe. Kristo alisema, “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu” Huu siyo muungano wa mara kwa mara. Tawi huwa sehemu ya mzabibu ulio hai. Yesu alisema Uhai mliopokea kutoka kwangu unaweza kudumishwa tu kwa muungano wa kudumu. Pasipo Mimi ninyi hamwezi kushinda dhambi, au kupinga majaribu. Lazima sisi tushikamane na Yesu na kupokea hali ya tabia yake kamilifu kwa imani.TVV 383.2

    Mzizi hupeleka lishe yake kupitia tawi hadi kijiti cha mwisho. Hivo Yesu alisema, “akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyu huzaa sana maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Tunapoishi kwa imani katika Mwana wa Mungu, matunda ya Roho yataonekana maishani mwetu; hakuna hata moja litakalokosekana.TVV 383.3

    “Baba yangu ndiye Mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa.” Kuna uwezekano wa kuonekana kuungana na Yesu bila muungano halisi pamoja naye kwa imani. Kule kukiri dini huwawezesha watu kuwemo kanisani, lakini tabia itaonyesha ikiwa wanao mwuungano mkamilifu na Kristo. Ikiwa hawazai matunda yo yote basi wao ni matawi ya uongo. Kristo alisema “Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya kuyatupa motoni yakateketea.”TVV 383.4

    “Na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.” Kutoka katika wanafunzi kumi na wawili waliomfuata Yesu, mmoja kama tawi lililonyauka alikuwa karibu kuondolewa; na waliobaki walikuwa karibu kupitia chini ya kisu kisafishacho cha tanuru kali. Kupogolewa (kupunguza yasiyofaa) huumiza, lakini Baba ndiye anayepogoa. llapogoi kwa mkono wa kuumiza. Majani mengi yanayozidi na kutumia rutuba na hivyo kuhatarisha matunda lazima yaondolewe na kutupwa mbali.TVV 383.5

    Majani yote kufunika lazima yaondolewe ili yasibane tawi lizaalo; na kulizuia kupata miali ya Jua la Haki. Mkulima huondoa yale majani yanayozuia kukua kusudi matunda yawe mengi zaidi. “Hivyo hutukuzwa Baba yangu.” Yesu akasema, “kwa vile mzaavyo sana.” Mungu hutamani kujidhihirisha kupitia kwenu utakatifu, ukarimu na huruma ya tabia yake Mwenyewe. Hata hivyo Mwokozi hakuwalazimisha wanafunzi wake wafanye kazi ya kuzaa matunda. Ila huwaambia tu kukaa wao ndani yake. Kwa njia ya Neno Kristo hukaa ndani ya wafuasi wake. Maisha ya Kristo ndani yako huzaa matunda sawa sawa na ya Kristo. Kuishi ndani ya Kristo, kumfuata, ukisaidiwa na Kristo, ukipata rutuba kutoka kwake, utazaa matunda yanayofanana na Kristo.TVV 383.6

    Amri ya kwanza kabisa Yesu aliyotoa alipokuwa na wanafunzi wake peke yao katika chumba cha ghorofa ilikuwa “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi nanyi mpendane vivyo hivyo.” Amri hii ilikuwa mpya kwa wanafunzi maana walikuwa hawapendani kama Kristo alivyowapenda. Lakini kwa njia ya maisha yake na kifo chake, wangepata maana mpya ya upendo Amri ya kupendana ilikuwa na nuru mpya kufuatana na kafara yake ya kujitolea.TVV 384.1

    Watu wanaposhikana pamoja kwa upendo wala si kwa kulazimishwa, huonyesha kutenda kazi kwa mvuto ulio juu kuliko kila mvuto wa kibinadamu. Huonyesha kuwa sura ya Mungu inaumbika ndani ya ubinadamu. Upendo wa jinsi hii ukionekana kanisani, utaamsha ghadhabu ya Shetani. “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyepeleka. Injili itahubiriwa katika hali zote, katikati ya upinzani, hatari, hasara, na mateso.TVV 384.2

    Kama Mwokozi wa ulimwengu, Kristo alikabiliwa na uwezekano wa kushindwa dhahiri. Alionekana kuwa anatenda kidogo tu kuhusu kazi aliyotamani kukamilisha. Mivuto ya Shetani ilikuwa akimletea mapingamizi daima. Lakini hakukata tamaa. Kwa njia ya Isaya amesema, “Nimeiitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.” Isaya 49:4.TVV 384.3

    Yesu alisimama katika Neno hili na hakumpa Shetani nafasi. Wakati huzuni kuu ilipoikabili nafasi yake aliwaambia kwa wanafunzi wake; “kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu wala hana kitu kwangu.” “Yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.” Sasa . . . atatupwa nje. (Yohana 14:30; 16:11; 12:31.)TVV 385.1

    Knsto alijua kuwa, atakaposema “Imekwisha”. mbingu yote itashangilia. Sikio lake lilisikia kwa mbali nyimbo na shangwe kuu iliyokuwa ikifanywa huko mbinguni kushangilia ushindi. Alijua kuwa jina la Kristo litatangazwa katika sayari zote na kutukuzwa. Alijua kuwa ukweli ulioimarishwa na Roho Mtakatifu utashinda katika vita dhidi ya uovu. Alijua kuwa maisha ya wanafunzi. wake waaminifu yatafanana na maisha yake, mfulululizo wa ushindi ambao haujapata kuonekana hapa lakini utakaotambulikana, hivyo katika siku ile kuu. Kristo hakushindwa wala kukata tamaa, na wafuasi wake wanapaswa kudhihirisha imani stahimilifu. vivyo hivyo. Waishi kama alivyoishi yeye na kufanya kazi kama alivyofanya. Badala ya kusikitikia matatizo, wakabiliane nayo na kushinda kukata tamaa.TVV 385.2

    Kristo alikusudia kuwa utaratibu wa mbinguni na ushirikiano wa Uungu mbinguni vionekane katika kanisa lake hapa duniani. Ili kwa njia ya watu wake apokee utukufu mwingi. Kanisa lililojaliwa na haki ya Kristo, ndiyo ghala yake ambao utajiri wa neema yake na, upendo wake vitaonekana kwa dhahiri. Kristo huwaangalia watu wake katika usafi na utimilifu wao kama tunu ya unyenyekevu wake na nyongeza ya utukufu wake.TVV 385.3

    Kwa maneno mazito na ya tumaini Mwokozi alimalizia mafundisho yake. Alikuwa amekamilisha kazi aliyopewa kufanya. Alikuwa amelidhihirisha jina la Baba na kujikusanyia wale ambao wangeendeleza kazi yake miongoni mwa wanadamu.TVV 385.4

    Knsto sasa kama Kuhani Mkuu Aliyewekwa wakfu aliwaombea watu wake, “Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.” “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.. Wote wawe na umoja; “ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.”TVV 385.5

    Knsto aliliweka kanisa lake teule mikononi mwa Baba. Kwake kulibakia vita ya mwisho na Shetani, naye alitoka kwenda kukabiliana navyo.TVV 385.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents