Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    74 — Pambano la Kutisha Katika Gethsemane

    Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika bustani ya Gethsemane. Mwezi wa majira ya Pasaka ulikuwa uking’aa sana kwa vile hapakuwepo na mawingu. Alipokaribia Gethsemane, alinyamaza kimya kwa hali isiyo ya kawaida. Katika maisha yake yote hapa duniani alikuwa akitembea katika nuru ya kuwepo Mungu. Lakini sasa alihesabiwa pamoja na wakosaji. Hatia ya wanadamu wote wa ulimwengu walioanguka lazima aibebe. Uzito wa hatia hii ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba alijaribiwa na kuogopa kuwa utamtenga milele na upendo wa Baba yake. Akapaza sauti, “Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa.”TVV 386.1

    Kamwe wanafunzi walikuwa hawajapata kumwona Mwalimu wao akiwa na huzuni kiasi hicho. Mwili wake ulipepesuka kana kwamba alikuwa anataka kuanguka. Walipofika bustanini, wanafunzi walianza kutafuta pale mahali pake pa faragha, kusudi Bwana wao apate kupumzika. Mara mbili wanafunzi wake walimsaidia, la sivyo angeanguka.TVV 386.2

    Walipofika karibu na mahali pa kuingilia, Yesu aliwaacha wanafunzi wengine na kuingia na watatu akiwasihi wajiombee na kumwombea pia. Akiwa pamoja na Petro, Yakobo na Yohana aliingia ndani zaidi sehemu za faragha. Katika pambano hili kuu, Kristo aliwahitaji wawe karibu naye. Mara nyingi walipitisha saa za usiku pamoja naye mahali hapa. Baada ya kipindi cha maombi walikuwa wakilala bila usumbufu mpaka asubuhi alipowaamsha kwenda kutenda kazi upya. Sasa aliwahitaji wakeshe pamoja naye katika maombi, walakini hakuweza, kustahimili hata washuhudie maumivu makuu yaliyomkabili.TVV 386.3

    Yesu alisema: “Kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.” Alisogea mbali kidogo, ila siyo mbali sana waweze kumwona na kumsikia, akaanguka chini kifudifudi. Alijisikia kuwa kwa sababu ya dhambi alikuwa anatengwa na baba yake. Shimo lilikuwa pana sana, jeusi sana, lenye kina kirefu sana kiasi kwamba roho yake ilitetemeka mbele yake. Maumivu haya hapaswi kutumia uwezo wa kimbingu ili kuyaepuka. Kama mwanadamu ni lazima apate adhabu ya matokeo ya dhambi ya mwanadamu. Kama mwanadamu lazima astahimili ghadhabu ya Mungu dhidi ya uasi.TVV 387.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents