Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jaribu la Kutisha

    Sasa Kristo alikuwa anasimama katika hali tofauti kabisa kuliko alivyokuwa kwa wakati wote uliopita. Kristo akiwa badala ya mwanadamu alikuwa anachukua adhabu chini ya hukumu ya Mungu. Mpaka hapo alikuwa mtetezi wa wengine; sasa alitamani kupata mtetezi kwa ajili yake mwenyewe.TVV 387.2

    Huku Kristo akijisikia kuwa mwungano kati yake na Baba yake umekatika, aliogopa kwamba hangeweza kustahimili pambano lile akiwa katika hali ya kibinadamu. Shetani alikuwa amekuja kwa pambano la kutisha mwisho; kama akishindwa, ufalme wa dunia hatimaye utakuwa wa Kristo, na yeye mwenyewe atapinduliwa. Lakini ikiwa Kristo atashindwa, dunia itakuwa ufalme wa Shetani na wanadamu watakuwa chini ya mamlaka yake milele.TVV 387.3

    Shetani alimwambia Kristo kuwa ikiwa atakuwa mdhamini kwa ajili ya ulimwengu wenye dhambi, atahesabiwa mmoja katika ufalme wa Shetani, na kamwe hatakuwa na uhusiano na Mungu tena. Na sasa kafara hii itakuwa na faida gani? Shetani alizidi kusisitiza hali ilivyo kwa Mkombozi; Akasema, watu wanaojidai kuwa ni matajiri wa mambo ya kiroho kuliko wengine wote wanataka kukuangamiza. Mmoja katika wanafunzi wako atakusaliti. Mmoja katika wanafunzi wako wakereketwa atakukana. Wote watakuacha. Kwamba wale Kristo aliowapenda mno watashirikiana na Shetani katika njama zake, kuliuchoma moyo wa Kristo. Pambano lilikuwa la kutisha mno. Dhambi za watu wote zilimlemea sana Kristo na kule kufahamu ghadhabu ya Mungu juu ya dhambi kulikuwa kunaponda uhai wake.TVV 387.4

    Katika uchungu wake alikumbatia ardhi, kama kujizuia asiondolewe mbali zaidi na Mungu. Kutoka katika midomo iliyokauka kulitoka kilio cha uchungu, “Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke, nisipokunywa mapenzi yako yatimizwe.”TVV 387.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents