Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  75 — Kesi Batili Dhidi ya Yesu

  Yesu aliharakishwa kupitia mitaa iliyokuwa kimya ya jiji lililokuwa limelala. Ilikuwa baada ya usiku wa manane. Akiwa amefungwa na kulindwa sana, Mwokozi alitembea kwa maumivu mpaka katika jumba la kuhani mkuu mstaafu, Anasi. Anasi alikuwa kiongozi wa jamaa ya ukuhani wa zamu, kwa kuwa alikuwa na umri mkubwa, watu walimheshimu kama kuhani mkuu. Shauri alilokuwa akitoa lilihesabiwa kana kwamba ni sauti ya Mungu. Kwa, hiyo ilimpasa awepo kwenye kumhoji mshitakiwa kwa sababu ya wasiwasi kwamba Kayafa ambaye ndiye kuhani mkuu hana uzoefu mkubwa hivyo angeshindwa kutekeleza kusudi lao. Hila na ujanja wake vilihitajika, maana Kristo lazima apatikane na hatia.TVV 393.1

  Kristo alikuwa ashitakiwe mbele ya Baraza kuu la Kiyahudi (Sanhedrin) lakini kwanza afikishwe mbele ya Annas kwa kuhojiwa. Chini ya sheria ya Kirumi, baraza kuu la Kiyahudi (Sanhedrin) lilikuwa na uwezo wa kuhoji na kisha kupitisha hukumu ambayo ilibidi kuthibitishwa na mamlaka ya Kirumi. Kwa hiyo ilibidi Kristo ashtakiwe na kosa ambalo lingeonekana kuwa la jinai mbele ya Warumi na pia mbele ya Warumi na pia mbele ya Wayahudi. Sio watu wachache waliongolewa na mafundisho ya Kristo, baina ya makuhani na wakuu. Yusufu wa Arimathaya na Nikodemo, hawataulizwa shauri hili, lakini wengine huenda wakathubutu kusema katika shauri hili. Lazima Sanhedrin liwe na umoja katika kusikiliza shauri dhidi ya Kristo. Makuhani walidhamiria kumshitaki kwa mambo mawili. Kama Yesu atathibitishwa kuwa ni mkufuru atahukumiwa na Wayahudi. Akithibitishwa kuwa ni mhaini, yaani mchochezi ili watu waasi serikali, atahukumiwa na Warumi.TVV 393.2

  Shitaka la pili Anasi alijaribu kulithibitisha kwanza. Alimhoji Yesu akitumaini kuwa atasema kitu fulani kitakachothibitisha alitaka kuanzisha chama cha siri kwa kusudi la kuanzisha ufalme wake. Na hivyo makuhani watamkabidhi kwa Warumi kuwa ni muanzishaji wa uasi. Kana kwamba anasoma mawazo ya ndani ya aliyemhoji. Kristo alikana kwamba hakukusanya watu kwa siri ili kuficha nia yake. Akasema “Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; siku zote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lo lote.”TVV 394.1

  Mwokozi alitofautisha jinsi ya kazi yake na mbinu za waliomshitaki. Walimwinda ili wampate na kumshitaki mbele ya mahakama ya siri ambapo wangepata kwa uongo kile ambacho wasingekipata kwa haki. Kule kukamatwa usiku wa manane na kundi la watu, dhihaka na matusi aliyokabili hata kabla ya kushtakiwa ilikuwa kawaida yao ya kutenda kazi na siyo yake. Kitendo chao kilikuwa ukiukaji sheria. Hata kanuni zao husema kuwa kila mtu anapaswa kuhesabiwa kuwa hana hatia mpaka athibitishwe kuwa ni mkosaji.TVV 394.2

  Yesu akimgeukia mshitaki wake, alisema: “Ya nini kuniuliza mimi? Je, wapelelezi hawakuwepo katika kila mkutano na kuwapa habari makuhani juu ya mambo aliyosema na kufanya?” Waulize wale waliosikia ni nini niliyowaambia; wao wanajua niliyonena.”TVV 394.3

  Anas alinyamazishwa kabisa. Mmoja wa maofisa watu wake alikasirika, akampiga Yesu usoni, akisema: “Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?” Kristo akamjibu kwa upole:TVV 394.4

  “Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini?” Jibu lake la upole lilitoka katika moyo wa usiokuwa na dhambi, mvumilivu na mwungwana; usiowezakuchokozeka.TVV 394.5

  Mikononi mwa viumbe ambavyo kwavyo, alikuwa anatoa kafara isiyo na kifani, Kristo alipokea kila aina ya dhalilisho. Na aliteseka kadiri ya utakatifu wake na chuki yake dhidi ya dhambi. Kuhukumiwa kwake na watu waliojifanya dhalimu ilikuwa kwake ni kafara ya milele. Kuzungukwa na wanadamu waliokuwa chini ya madaraka ya Shetani lilikuwa jambo la kuchukiza. Na alijua kuwa kwa kuutokeza ghafla uwezo wake na Uungu angewafanya watesi wake wote wakatili kuwa mavumbi. Hali watesi hii ilifanya mateso yake kuwa magumu sana kuvumilia.TVV 394.6

  Wayahudi walimtazamia Masihi atakayetumia Uungu wake kugeuza mtiririko wa mawazo ya watu na kulazimisha waukubali ukuu wake. Hivyo Kristo alipodhalilishwa, lilimjia kwa nguvu jaribu la kutaka kudhihirisha uwezo wa tabia yake ya Uungu, kuwashurutisha watesi wake kukiri kuwa alikuwa Bwana juu ya wafalme, watawala, makuhani na hekalu. Ilikuwa vigumu kudumisha hali aliyoichagua ya kama mmoja na wanadamu.TVV 394.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents