Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    21 — Bethzatha na Sanhedrin

    “Sasa katika Yerusalemu, penye mlango wa kondoo pana birika iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, wakingoja maji yachemke.”TVV 107.1

    Wakati fulani maji hutibuliwa katika birika, na iliaminiwa kuwa kuna uwezo usiokuwa wa kibinadamu, na kwamba mtu yeyote atakayetumbukia humo mara ya kwanza, ataponyeka ugonjwa wake. Watu wengi walikuwa wakingoja maji hayo; lakini watu walizidi sana, hata waliokuwa na nguvu walikuwa wakiwakanyaga wadhaifu, wakikimbilia kuponywa. Wengi waliweza kufika hapo walifia kwenye kingo zake kwa kukosa uwezo wa kuingia ndani. Kambi zilijengwa kando kando yake na kuwahifadhi wagonjwa. Baadhi ya wagonjwa walilala kando ya matao hayo wakingoja maji yatibuliwe.TVV 107.2

    Yesu alikuwako Yerusalemu tena. Akitembeatembea huko mwenyewe, akiwa na kusudi la kuomba, walifika kwenye dimbwi hilo. Akiwaona wagonjwa hao, alitamani kutumia uwezo wake wa kuponyesha, na kumponya kila mgonjwa. Lakini ilikuwa siku ya Sabato, naye alijua kuwa akitenda tendo la kuwaponya watu, ataleta fujo sana kwa Wayahudi, na atakatiza kazi yake kabla ya wakati.TVV 107.3

    Walakini Mwokozi alimwona mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa zaidi ya wote, mtu ambaye amekuwa hawezi, kwa muda wa miaka thelathini na minane. Ugonjwa wake ulihesabiwa kana kwamba ni adhabu kutoka kwa Mungu. Akiwa peke yake, bila msaada wowote, ni kana kwamba ametengwa mbali na huruma za Mungu. Mgonjwa huyu ameugua muda wa miaka thelathini na minane bila kuhurumiwa na mtu yeyote. Wakati maji yalipotibuliwa, watu waliomhurumia walimchukua kuelekea kwenye dimbwi. Lakini wakati huo inavyoelekea kutibuliwa kwa maji, hukosa mtu wa kumwingiza dimbwini. Kwa muda wote hakuweza kufika mbali zaidi ya ukingo wa dimbwi, Juhudi yake ya kuingia dimbwini na uchungu wa kukosa kuingia, vilimdhoofisha sana.TVV 107.4

    Mgonjwa alikuwa amelela katika kirago chake, wakati alipofikiwa na mtu mwenye uso wa huruma. Maneno yenye tumaini, kwamba: “Unataka kuwa mzima?” yalimsisimua. Alitumaini kuwa inawezekana kupata msaada. Lakini tumaini lake lilififia mara. Alikumbuka jinsi alivyokuwa akijaribu kila mara, na kushindwa. Akasema: “Bwana sina mtu wa kunisaidia, wakati maji yanapotibuliwa, kunitupa dimbwini, lakini wakati ninapojikakamua, mtu mwingine hutangulia mbele yangu kutumbukia dimbwini.”TVV 108.1

    Yesu hakumwambia mgonjwa huyu amwamini, ila tu alisema: “Inuka ujitwike kitanda chako uende.” Lakini imani ya mtu huyu ikamshikilia Yesu. Kila mshipa wake, na misuli yote ikapata uhai mpya. Akayaamini maneno ya Kristo, na kutii maagizo yake, kwa hiyo mishipa yote ikapata nguvu. Akaruka kwa miguu yake, akawa mtu mzima.TVV 108.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents