Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Watu wamkusanyikia Yesu

  Katika mojawapo ya unabii unaomhusu Yesu, iliandikwa: “Fimbo ya enzi haitaondoka kutoka kwa Yuda, wala mtoa sheria katikati ya miguu yake, mpaka Shilo ajapo, na kwake mataifa yatakusanyika.” Mwanzo 49:10. Watu walikuwa wanakusanyika kwa Kristo. Kama makuhani na marabi wasingekuwa wanaingilia, mafundisho yake yangalileta mabadiliko ya ajabu ambayo hayajaonekana. Lakini wakuu hawa walikusudia kuharibu mvuto wa Yesu. Mipango waliyokuwa wakipanga katika Sanhedrini, na malaumu ya waziwazi juu yake, vingesaidia kuvunja mvuto wake. Mtu yeyote aliyethubutu kumlaumu Rabi, alihesabiwa kama mhaini. Kwa jambo hili marabi walitumaini kuchochea fitina juu ya Yesu alipokuwa akijaribu kuzikanusha desturi za marabi, na hivi wakaleta mgawanyiko katika watu, na kuandaa njia ya kuwa chini ya utisho wa Warumi.TVV 110.1

  Baada ya Shetani kushindwa kumwangusha Yesu jangwani, alijikusanya tena apate kumdhoofisha Yesu na kazi yake. Aliwapofusha Wayahudi wasimtambue Yesu kuwa ndiye Mwokozi, wakaungana na waongozi wao, wakimhesabu mkuu wa ukweli kuwa ni adui yao. Akawafanya wamkane Kristo, na kumwudhi daima. Kwa njia hiyo wangalimkatisha tamaa na kuvuruga kazi yake.TVV 110.2

  Yesu alikuja kuitukuza sheria, na kuifanya iheshimiwe. Isaya 42:21. Alikuja kuifungua Sabato kutokana na mambo ya kiutumwa watu waliyoiwekea, mpaka” ikaonekana kuwa ni laana badala ya kuwa baraka. Kwa ajili ya hayo aliamua kuponya mgonjwa siku ya Sabato, huko Bethzatha. Angeweza kuponya mgonjwa siku nyinginezo, au angemponya bila kumwagiza ajitwike kitanda chake. Lakini alichagua njia hiyo na kumwambia mtu ajitwike kitanda apite wazi akionwa na kila mtu katika siku hiyo. Jambo hili lingeonyesha kuwa anakanusha mambo ya marabi na sheria mbaya juu ya Sabato, ambayo ni siku ya Bwana.TVV 110.3

  Yesu alitangaza kuwa kumponya tu mwenye dhiki siku ya Sabato ni tendo halali kabisa kufanywa siku ya Bwana. Malaika wa Mungu daima huwahudumia wanadamu. “Baba yangu hufanya kazi siku zote, vivyo hivyo na mimi nafanya kazi.” Siku zote ni za Mungu za kuendeshea mpango wa wokovu kwa ajili ya wanadamu. Kama Wayahudi wangetafsiri na kuieleza sheria kikamili, ndipo aliyeiumba sabato angefanya nafasi katika kazi yake, na angekomesha mzunguko wa ulimwengu ambao hauna mwisho.TVV 110.4

  Je, Mungu angekataza jua lisifanye kazi yake siku ya Sabato? Je, azuie vijito vya maji visifurike kunywesha nchi siku ya Sabato? Je, azuie ngano na mahindi kukua siku ya sabato? Je, miti na maua visichanue siku ya Sabato?TVV 110.5

  Mungu asingeweza kuzuia mkono wake usifanye kazi hata nukta moja, ama sivyo, watu na viumbe hai vingezimia na kufa. Mwanadamu pia anayo kazi impasayo kufanya siku ya Sabato. Wagonjwa lazima wahudumiwe, mahitaji ya lazima budi yatolewe. Siku takatifu ya Mungu ya kupumzika ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu. Mungu hataki viumbe vyake viwe na taabu hata saa moja, ila lazima vishughulikiwe, siku ya Sabato.TVV 111.1

  Amri ya Sabato hukataza kufanya kazi za kawaida siku hiyo, kazi za kujishughulikia ili upate riziki, lazima zikome. Hakuna kazi za kujipatia mapato zinazokuwa halali kufanyika. Lakini kama vile Mungu alivyoacha kufanya kazi siku hiyo, na kustarehe katika Sabato, vivyo hivyo mtu pia afanye kazi siku sita, na kustarehe siku ya Sabato. Sabato ni ya kuabudu, na kutenda matendo matakatifu.TVV 111.2

  Lakini Mafarisayo walikuwa wakichukiza zaidi. Yesu hakuvunja sheria tu, jinsi wao walivyodhani, lakini kwa kumwita Mungu ni “Baba yake”, alijitangaza kuwa sawa na Mungu. Walimlaumu kuwa anakufuru. Maadui hawa wa Kristo, waliziita kanuni zao na desturi zao kuwa ni mambo ya dini. Hizi zilionekana kuwa hazifai kitu kulinganisha na maelezo ya Yesu ya kutoka katika Neno la Mungu, na kufuatana na hali ya ulimwengu katika mzunguko wake usiokuwa na mwisho. Lakini Marabi walipotosha maelezo yake, wakawachochea watu wamchukie kwa kuwa anajifananisha na Mungu. Kama makuhani na marabi wasingekuwa wanaogopa watu wangalimwua mara moja. Lakini mvuto wake kwa makutano ulikuwa mkubwa sana. Wengi waliona kuwa kumponya mgonjwa wa Bethzatha ilikuwa sawa kabisa.TVV 111.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents